Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko akiambatana na kamati ya Ulinzi na usalama Mkoani hapa amefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo katika wilaya ya Mpanda kwa lengo kuhakikisha miradi inayotekelezwa inazingatia viwango vinavyotakiwa na kwa wakati, ili kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Ziara hiyo imefanyika leo Juni 25, 2025 ambapo ametembelea ujenzi wa kituo jumuishi cha kutoa haki, hospital ya rufaa, shule ya wasichana Katavi pamoja na shule ya amali katika kijiji cha Tumaini ambapo pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi amesisitiza uwajibikaji ili kupeleka huduma bora za kijamii kwa wananchi.
Mhe. Mrindoko amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipambanua kwa kusogeza huduma karibu na wananchi, hivyo ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa ubora na tija.
"Tumekagua miradi hii na tumeridhishwa na utekelezaji wake kikubwa cha kusisitiza ni kwamba ukamilishaji wa miradi hii ufanyike kwa haraka pamoja na kuhakikisha kuwa watumiaji wa miundombinu hii wanatumia bila kuwa na changamoto.ambazo zinaweza kuwa kikwazo," Amesema Mh. Mrindoko.
Ziara ya hii imeonyesha dhamira ya dhati ya serikali ya mkoa wa Katavi katika kuhakikisha maendeleo yanamgusa kila mwananchi. Mhe. Mrindoko aliwahakikishia wananchi kuwa mkoa utaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi yote ya maendeleo ili kuleta mabadiliko chanya ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa Katavi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi
Telephone: 025-2957108
Mobile:
Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.