• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

RC Katavi,amuomba Waziri wa Maji kuingilia kati kusuasua Ujenzi Bwala la Nsenkwa Mlele, Atoa onyo kwa Mkandarasi.

Posted on: August 28th, 2022

Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Bwala la Maji Nsenkwa kutoka kwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mlele Bw.Gilbert Isack wakati alipofanya ziara kukagua Mradi huo wa Maji.

Mlele -Katavi 

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amemuomba Waziri wa Maji pamoja na RUWASA Makao makuu kusaidia kutatua changamoto zinazosababisha  kusua sua kwa ujenzi wa Bwala la Maji Nsenkwa lililopo katika Kijiji cha Nsenkwa Kata ya Nsenkwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ili Wananchi waondokane na changamoto ya Uhaba wa  Maji.

Ujenzi wa Bwawa hilo la Maji linalotegemewa kuondoa adha ya Maji kwa  Wakazi wa takribani  Vijiji 16 katika  Wilaya ya Mlele umeendelea kusuasua kumalizika kwa takribani miaka 4 ikiwa ni tangu kuanza utekelezaji wake Mwaka 2018.

Akizungumza wakati wa Ziara yake 27 Agosti 2022 kukagua mradi huo wa Maji Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema licha ya changamoto ya mawasiliano  iliyowasilishwa na uongozi wa RUWASA ngazi ya Wilaya katika Taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mradi huo  bado kuna changamoto ya Mkandarasi kutokuwa makini katika utekelezaji wa mradi huo.

“Nimeona hapa kuna matatizo ya aina mbili la kwanza ni kwa Mkandarasi Mwenyewe yaani spidi yake sio nzuri,hajajipanga nampa Onyo kupitia  RUWASA Mkoa pamoja na RUWASA Makao makuu wamsimamie huyu ili aweze kutekelza makubaliano ya mkataba na sio kuleta visingizio”alisema RC Mrindoko.

Mhe.Mrindoko amebanisha kuwa changamoto nyingine ni RUWASA Makao makuu  wenyewe ambao  wamekuwa chanzo cha kusuasua mradi huo kutokana na kuchelewa kujibu Burua ambazo mara kadhaa wamekuwa wakiandikiwa na RUWASA Ngazi ya Mkoa.

“Nimesikia hapa barua zinaandikwa mawasiliano yanafanyika na RUWASA Makao makuu lakini hawajibu chochote. Niombe RUWASA Makao makuu niombe Wizara ya Maji, Vijiji 16 vina changamoto ya Maji hapa Mlele kwa sababu mradi huu haukamiliki kwa wakati hatuwezi kuendelea namna hii.”alisema RC Mrindoko.

Kutoka na changamoto hiyo Mhe.Mrindoko ametoa Ombi kwa RUWASA Makao Makuu pamoja na Wizara ya Maji kufika katika Mradi huo kutatua changamoto zilizopo ili Wananchi waondokane na changamoto ya upatikanaji wa Maji katika Wilaya ya Mlele.

Aidha Mhe.Mrindoko pia ametoa maelekezo kwa RUWASA Mkoa wa Katavi kumsimamia kwa karibu Mkandarasi HEMATEC Investment LTD    anayeteleleza mradi huo ili aweze kutekeleza mradi huo kwa viwango na ubora unaotakiwa.

Kwa Upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mlele Bw.Gilbert Isack ameeleza kuwa mradi huo ambao utazalisha Lita Bilioni 2 za Maji kwa mwaka  kwa sasa uko katika hatua za Mwisho za ukamilishaji ambapo pindi mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.8 utakapokamilika utaondoa adha ya Maji kwa wakazi takribani 68,000 kwa Vijiji 16 Wilayani Mlele.

MATUKIO KATIKA PICHA 

Picha 1:Muonekano wa Bwawa la Nsenkwa lililoko Kijiji cha Nsenkwa Kata ya Nsenkwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele linalotegemewa na Wakazi wa Wilaya ya Mlele kama chanzo kikuu cha Maji.


Picha 2:Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Philberto Sanga akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko alipotembelea Mradi wa Maji wa Bwawa la Nsenkwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele 27 Agosti 2022.


Picha 3:Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa akiomba ufafanuzi kutoka kwa Mwakilishi wa Mkandarasi Kampuni ya HEMATEC Investment LTD inayoteleleza Ujenzi wa Mradi wa Bwala la Nsenkwa katika Ziara ya RC Katavi kukagua Miradi 27 Agosti 2022.


Picha4:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrondoko akipokea maelezo kuhusu Mradi kutoka kwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mlele alipotembelea mradi wa Maji wa Ujenzi wa Bwawa la Nsenkwa 27 Agosti 2022



 Picha 5:Mwakilishi wa Kampuni ya HEMATEC Investment inayotelekeza Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Nsenkwa akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko katika ziara hiyo 27 Agosti 2022


Picha 6:Meneja wa RUWASA Mkoa wa Katavi akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Bwawa la Nsenkwa.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • BARAZA MAALUM LA MADIWANI TANGANYIKA LAJADILI TAARIFA YA CAG, WATUMISHI WATAKIWA KUFUATA SHERIA.

    June 17, 2025
  • RAS MSOVELA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE.

    June 19, 2025
  • MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO AFRIKA, CHAGULAGA BADO NI KILIO KWA WASICHANA KATAVI.

    June 16, 2025
  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.