• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

RC Katavi awaonya Wafanyabiashara Vyuma Chakavu.

Posted on: June 2nd, 2022

Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akizungumza na mmoja wa Wafanyabiashara  wa duka katika kata ya makanyagio wakati wa ukaguzi wa utekelezaji  Zoezi la Uwekaji wa vibao vya namba katika Nyumba.

Na: John Mganga-Katavi- RS

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko ametoa onyo kwa Wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu kujihadhari na ununuzi wa vyuma vitokanavyo na miundombinu ya Serikali.

Mhe.Mrindoko ametoa onyo hilo kufuatia uwepo wa Taarifa za upotevu wa baadhi ya Vibao vya chuma vya anuani za makazi katika baadhi ya mitaa  katika Manispaa ya Mpanda.

Akizungumza Wananchi wa Kata ya Makanyagio mara baada ya kukagua utekelezaji wa zoezi endelevu la uwekaji wa vibao vya anuani za makazi Mhe.Mrindoko amesema ni jukumu la kila Mwananchi kulinda miundombinu ya Serikali kwa kuwa Serikali imewekeza fedha nyingi katika miundombonu hiyo.

Amesema hatua kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika kuhujumu miundombinu hiyo ya anuani za makazi huku akisisitiza kuwa Mfanyabiashara yoyote wa vyuma chakavu atakayebainika kujihusisha na ununuzi wa vyuma vitokanavyo na miundombinu ya serikali hatua kali zitachukuliwa dhidi yake ikiwa ni pamoja na kufungiwa kufanya biashara hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Mpanda Bi.Sophia Kumbuli amekiri kuwepo kwa upotevu wa baadhi ya vibao vya anuani za makazi katika baadhi ya maeneo ambapo ameeleza kuwa kama Manispaa wamechukua hatua ya kugharamia ununuzi wa Vibao hivyo na kuviweka katika baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na kadhia hiyo.

Bi.Kumbuli ametoa wito kwa Wananchi wa Manispaa ya Mpanda kutoa ushirikiano kwa Serikali kulinda miundombinu hiyo ambayo ina faida kubwa kwa Wananchi.

Nae Mstahiki Mea wa Manispaa ya Mpanda Mhe.Haidary Sumry ameipongeza Manispaa ya Mpanda kwa kutekeleza zoezi hilo kwa umakini mkubwa huku akiishukuru Serikali ambapo amesema ni muhimu kwa Viongozi kuendelea kuwaelimisha Wananchi kuhusu umuhimu wa zoezi la Anuani za Makazi pamoja na faida zake.

Kwa Upande wao baadhi Wananchi wa Makanyagio wameshauri Serikali kuendelea kutoa elimu kwa Wananchi juu ya faida za Mfumo wa anuani za makazi ili waweze kutumia fursa hiyo kurahisisha shughui za kiuchumi.

Zoezi la uwekaji mfumo wa anuani za makazi Mkoani Katavi limekamilika kwa Asilimia 100 ambapo licha ya changamoto kadhaa maendeleo ya zoezi endelevu la  uwekaji wa vibao katika Mitaa linaendela vizuri.

 

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

    June 09, 2025
  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.