• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

RAS MSOVELA AAGIZA MAAFISA BIASHARA KUSIMAMIA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA, MIKATABA YA WAWEKEZAJI NA ULINZI WA MAENEO YA UWEKEZAJI.

Posted on: June 26th, 2025

Kikao cha tathmini ya maendeleo ya sekta ya viwanda, biashara na uwekezaji kwa kipindi cha miaka mitano kimefanyika leo Juni 26,2025 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, kikihusisha maafisa biashara kutoka Halmashauri zote za mkoa pamoja na wadau wa sekta ya viwanda na biashara. Kikao hicho kimekuwa jukwaa muhimu la kupima hali ya biashara na uwekezaji, pamoja na kuweka mikakati ya kuboresha mazingira ya uchumi wa mkoa.

Katibu Tawala wa Mkoa, Bw. Albert Msovela, ameongoza kikao hicho na kubainisha kuwa bado kuna changamoto kubwa ya upatikanaji wa elimu kwa wafanyabiashara, hali inayowapelekea wengi wao kuendesha shughuli bila kuwa na leseni halali. Amesisitiza kuwa ni wajibu wa maafisa biashara kuhakikisha wanawafikia wafanyabiashara, kuwapatia elimu stahiki na kuwatengenezea mazingira rafiki ya kufanyia biashara.

Ameelekeza pia kufuatiliwa kwa karibu mikataba inayotolewa na wawekezaji, hasa kwenye sekta ya madini, ili kuhakikisha haibebi masharti kandamizi kwa wazawa. Amesema ni muhimu kulinda haki za wafanyakazi wa ndani katika maeneo yote ya uwekezaji.

Ametoa pongezi kwa TRA na Wakala wa Madini kwa juhudi zao za kuhakikisha ukusanyaji wa mapato unafanyika kwa uwazi na kwa kutoa taarifa za kila mwezi za utendaji wao. Amezitaka taasisi nyingine za umma kuiga mfano huo ili kuongeza uwajibikaji na kuimarisha huduma kwa wananchi.

Ameeleza pia kuwa maeneo mengi ya uwekezaji yamevamiwa, na amewataka maafisa biashara kuchukua hatua za haraka kukabiliana na hali hiyo kabla haijathiri zaidi mwelekeo wa maendeleo ya mkoa. Aidha, ameagiza mabaraza ya biashara kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuhakikisha vikao vinafanyika mara kwa mara kama ilivyoainishwa kwenye miongozo.

Ameomba Katibu Tawala Msaidizi, anayeshughulikia masuala ya viwanda na biashara, Bw. Florence Chrisant, kuratibu kwa karibu utoaji wa elimu endelevu kwa wafanyabiashara pamoja na kusimamia matumizi sahihi ya vipimo ili kuhakikisha biashara zinafanyika kwa haki na kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • RAS MSOVELA AAGIZA MAAFISA BIASHARA KUSIMAMIA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA, MIKATABA YA WAWEKEZAJI NA ULINZI WA MAENEO YA UWEKEZAJI.

    June 26, 2025
  • RC MRINDOKO ASISITIZA UWAJIBIKAJI KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO

    June 25, 2025
  • BARAZA MAALUM LA MADIWANI TANGANYIKA LAJADILI TAARIFA YA CAG, WATUMISHI WATAKIWA KUFUATA SHERIA.

    June 17, 2025
  • RAS MSOVELA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE.

    June 19, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.