Katika hotuba ya mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, aliyoitoa leo Julai 5, 2025 wakati wa tamasha la Samia, kumpongeza Mhe. Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha za Maendeleo na kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma za kijamii
Fedha hizo ni kwa ajili ya kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo, Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano na Mikakati mbalimbali ya Serikali.
Kufuatia utekelezaji huu wa miradi ya maendeleo timu ya vijana wa Dejong kutoka Kizimkazi Zanzibari wamefika ili kujionea namna ambavyo miradi hii imekuwa na msaada kwa jamii na kuchochea maendeleo ya kiuchumi.
Mratibu wa timu hiyo Hassan Hamdu akizungumza na wananchi katika tamasha hilo amesema ujio wao umelenga kuwaonyesha wananchi wa mkoa wa Katavi umuhimu wa uwepo wa miradi ya kimkakati katika jamii hususani katika nyaja za afya, Elimu, Uchumi, usafirishaji pamoja na miradi mingine.
Aidha amesema katika upande wa elimu ni Fursa kwa wananchi kuweza kutumia miundombinu iliyopo kwa watoto kupata nafasi ya kusoma na kufikia malengo ya serikali ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. mwanamvua Mrindoko akizungumza katika tamasha hilo amesema hadi kufikia Juni, 2025 Mkoa una jumla ya Shule za Msingi 293, ambapo kati ya hizo za Serikali ni 278 na zisizo za Serikali ni 15,Shule za Sekondari zipatazo 79 zikiwemo 74 za Serikali na 5 ni Shule za binafsi, Sekta ya Elimu imepokea kiasi cha Sh Bilioni 58.093 zilizotumika katika kuboresha miundombinu ya Shule mbalimbali na kuweka mazingira mazuri ya kufundishia na kujifunza.
Pia Katika hotuba yake, Mhe. Mrindoko Amesema Kuna Ujenzi wa Shule mpya 137 zikiwemo Shule 97 za Msingi na Shule 40 za Sekondari, na madarasa 2,219 madarasa. Hali ambayo imepunguza umbali wa kutembea kwenda Shule na msongamano wa Wanafunzi madarasani na kuwezesha mazingira bora zaidi kwa walimu na wanafunzi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi
Telephone: 025-2957108
Mobile:
Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.