• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Mpanda Manispaa Yaonesha Njia Nane nane 2018

Posted on: August 3rd, 2018

Mkoa wa Katavi unaendelea na mkakati wake wa kuwawezesha Wajasiliamali kutambua fursa zaidi za uwekezaji na masoko katika maonesho ya Nane nane Jijiji Mbeya. Mkuu wa Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji toka Sektretariet ya Mkoa wa Katavi Mhandisi Awariywa Nnko, amewaeleza washiriki wa Maonesho ya Nane nane katika Banda la Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuwa azma ya Mkoa wa Katavi ni kuyafanya maonesho ya nane nane mwaka 2018 kuwa ya Kilimo biashara ili yawe chachu ya mabadiliko kwa washiriki wa Mkoa wa Katavi  na kuona Kilimo ni shughuli inayoweza kuboresha maisha yao. Aidha Mhandisi huyo wa Kilimo amewaambia washiriki kuwa sasa muda umefika kwa washiriki kuwa wabunifu na kujifunza teknolojia mbalimbali zinazooneshwa katika viwanja vya nane nane Jijini Mbeya na kuchukua hatua ya kuanzisha viwanda katika maeneo yao wanayotoka. “ Itapendeza na itakuwa faraja kwa wanakatavi kuona wajasiliamali walioshiriki katika maonesho haya mwaka huu 2018, mwakani wakija katika maonesho kama haya wanakuja kuonesha bidhaa zilizozalishwa na viwanda vipya walivyoanzisha wenyewe kama walivyofanya wenzetu wa Katavi Dairy Milk na RK kutoka katika Manispaa ya Mpanda, ambao tumeshuhudia wakionesha bidhaa zao zilizoongezwa thamani”.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Manispaa ya Mpanda Bibi Marietha Mlozi, amesema Halmashauri yake imejipanga  kuhakikisha kuwa washiriki kutoka Manispaa ya Mpanda wanapata fursa ya kuonesha bidhaa zao na kutafuta masoko ya kudumu ya bidhaa wanazozalisha, na kubwa zaidi kujifunza kwa kina teknolojia za kilimo zinazooneshwa na taasisi na mashirika ambazo zitawasaidia kuongeza uzalishaji katika kilimo, mifugo na uvuvi. Mkuu huyo wa Idara amewaambia washiriki kuwa Halmashauri yake imejipanga kwa mwaka huu kuhakikisha inafanya vizuri katika maonesho haya, na kusema kuwa wameandaa rejista muhimu ya wajasiliamali na wakulima waliokuja kujifunza kutoka katika Halmashauri yake, rejista hiyo itatumika kuhakikisha kuwa wanamfatilia mshiriki mmoja mmoja kuona maendeleo yake baada ya kujifunza katika maonesho haya.

Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw.Donald amewaambia washiriki wenzake kuwa kila mtu kwa nafasi yake ajitume na ahakikishe anafanya kazi kwa bidii, ili kuhakikisha wanapata ushindi katika maonesho ya mwaka huu 2018, kwani Manispaa ndiyo Kioo cha Mkoa wa Katavi, hivyo Mnispaa ikifanya vizuri, Mkoa wote pia unakuwa umefanya vizuri.

Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika maonesho ya Nanenane mwaka 2018, imejipanga kuhakikisha inafanya vizuri na kuongoza katika maeneo yote.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

    June 09, 2025
  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.