• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Wafanyakazi Katavi waaswa kujiepusha na Rushwa,Wahimizwa kuchapa kazi kuleta Maendeleo.

Posted on: May 1st, 2022

Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi 2022, Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh.Filberto Sanga(Aliyevalia Suti Katikati) kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi akipokea maelezo kuhusu namna  ya kurekebisha Mfumo wa Gurudumu za Gari  kwa kutumia Mfumo wa Kompyuta kutoka kwa Mkufunzi  wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA-Mpanda alipotembelea Banda la maonyesho katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Mei Mosi 2022 yaliyofanyika katika Uwanja wa  Kashaulili  Manispaa ya Mpanda.


Na: John Mganga-IO-Katavi RS

Wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma yakiwemo mashirika pamoja na Taasisi  Binafsi Mkoani Katavi wameungana na Wafanyakazi wenzao kote Nchini na Duniani kwa Ujumla  kuadhimisha Sikukuu ya Wafanyakazi Duniani Mei mosi.

Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo,Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh.Filberto Sanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko ameongoza Wafanyakazi katika kusherehekea Siku hiyo muhimu ya Wafanyakazi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mh.Sanga ametoa wito kwa Wafanyakazi Mkoani Katavi kuongeza bidii katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu pamoja na kuzingatia Sheria kanuni na Taratibu za Ajira ili kuliletea Taifa maendeleo.

Ameeleza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa Wafanyakazi katika Sekta mbalimbali Nchini  na kwamba itaendelea kuhakikisha kuwa inasimamia na kulinda maslahi mapana ya Wafanyakazi pamoja na kuboresha stahiki mbalimbali kwa wafanyakazi ili waweze kuleta tija iliyokusudiwa.

Mh.Sanga amewataka Watumishi wa Umma ambao wamekabidhiwa dhamana kubwa ya kutoa huduma kwa Wananchi  kujihadhari na tabia na vitendo  mbalimbali vinavyoshusha hadhi ya Watumishi wa Umma jambo linaloichafua Serikali.

Amezitaja tabia hizo kuwa ni pamoja na Lugha chafu wakati wa kuhudumia Wananchi,tabia mbaya ya kuomba rushwa ambapo amesisitiza kuwa Serikali haitosita kuchukua hatua a kinidhamu kwa wale wote watakaobainika kuendeleza vitendo hicyo visivyokubalika katika Jamii.

Awali katika Risala ya Wafanyakazi iliyosomwa na uwakilishi kutoka vyama vya Wafanyakazi Mkoani Katavi imeelezwa kuwa watumishi bado wanakabiliwa na changamotyo mbsalimbali jambo linaloathiri kwa sehemu kubwa Utendaji kazi kwa watumishi wa Umma

Aidha wafanyakazi wameiomba serikali kuborsha kuendelea kuboresha maslahi mbalimbali kusudi kuleta tija katika utumishi wa Umma.

Katika Maadhimisho hayo yanayofanyika kila Mwaka Mh.Sanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Hozza Mrindoko amekabidhi Zawadi mbalimbali kwa Wafanyakazi kutoka Taasisi mbalimbali za Umma na Binafsi ili kuamsha ari kwa Wafanyakazi

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

    June 09, 2025
  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.