• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Katibu Tawala Katavi awataka Watumishi Tanganyika kudumisha mahusiao mema kazini.

Posted on: September 5th, 2022

Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa amewaasa watumishi Wilayani Tanganyika kudumisha ushirikiano na mahusiano mema kazini ili kufikia malengo mahsusi ya Serikali ya utoaji huduma bora kwa Wananchi.

Katibu Tawala Rugwa ametoa rai hiyo alipozungumza na Watumishi wa Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Tanganyika katika ziara yake Wilayani humo Septemba 5, 2022 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,ikiwa ni sehemu ya ratiba yake kukutana na kuzungumza na watumishi wa kada mbalimbali Mkoani Katavi kwa lengo la kujitambulisha ikiwa ni muda mchache tangu kuwasili Katavi akitokea Kituo chake cha awali Dar Es Salaam.

Bw.Rugwa amewaambia watumishi wa Tanganyika  kuwa kutokana na Watumishi wa Umma kutumia muda mwingi mahala pa kazi kuliko maeneo mengine ni muhimu kudumisha mahusiano mazuri kazini kwa kupendana na kuthaminiana  ili kuboresha mazingira ya kazi jambo ambalo litasaidia kwa sehemu kubwa kufikia malengo mahsusi ya Serikali ya utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.

Katibu Tawala Rugwa ameahidi ushirikiano wa kutosha kwa watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika akiwataka kutosita kufika ofisini kwake iwapo kuna changamoto yoyote ya kiutumishi inayowakabili watumishi hao.

Aidha Bw.Rugwa ameongeza kuwa ni furaha yake kuona watumishi wa Umma  Mkoani humo wanapiga hatua kimaendeleo na kufikia malengo yao jambo ambalo linaleta Afya katika utumishi wa Umma.

“Kwa hiyo mimi matarajio yangu ni kuwa licha ya kuwa kiongozi naahidi kuwa mlezi mzuri wa watumishi,Katavi ni sehemu nzuri sana ya Watumishi kufikia matarajio yao”

Katibu Twala Rugwa pia ameongeza kuwa Mkoa wa Katavi ni moja kati ya mikoa Nchini inayokua kwa kasi zaidi ukilinganisha na mikoa mingine iliyoanzishwa miaka ya karibuni hivyo ni vema Watumishi wakatizama fursa za kuchumi zilizopo na kuzitumia ili kufikia malengo mahsusi ya kujiletea maendeleo.

Kwa Upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Bw.Betuely Ruhega ameeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika licha ya mafanikio makubwa iliyoyapata bado   inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa watumishi pamoja na Vitendea kazi ambapo amemuahidi Katibu Tawala Mkoa kuwa wanaendelea na jitihada za kutatua changamoto hizo.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • BARAZA MAALUM LA MADIWANI TANGANYIKA LAJADILI TAARIFA YA CAG, WATUMISHI WATAKIWA KUFUATA SHERIA.

    June 17, 2025
  • RAS MSOVELA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE.

    June 19, 2025
  • MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO AFRIKA, CHAGULAGA BADO NI KILIO KWA WASICHANA KATAVI.

    June 16, 2025
  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.