Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Tanganyika kwa utekelezaji mahili wa miradi ya kimikakati inayoendelea wilayani hapo kutokana na mapato ya ndani ya biashara kaboni.
Akizungumza katika Baraza maalumu la madiwani lililoketi leo Mei 13, 2025 kwa ajili ya kujadili taarifa za utekelezaji wa miradi ya Bakaa inayoendelea na miradi ya kimikakati katika halmashauri ya wilaya Tanganyika amesema miradi mingi imetekelezwa na kukamilika na inaketa manufaa kwa wananchi wa halmashauri hiyo.
Picha: Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko akizungumza katika
baraza maalumu la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika.
"Kupitia biashara ya kaboni mmebuni miradi mingi kwakweli hongereni sana, tunaamini halmashauri hii itakuwa mfano wa kuigwa ndani ya mkoa wa Katavi na hata nje ya mkoa na kuwa sehemu ya kujakujifunza kuhusu masuala ya kaboni," amesema Mh. Mrindoko.
Picha: Baadhi ya wajumbe wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani.
Akitoa taarifa ya hali halisi ya uwekezaji wa miradi ya kimikakati afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya Tanganyika Deus Luziga amesema vijiji kupitia mapato yake ya awamu ya Tisa na Kumi vilitenga jumla ya Shs. 436,000,000.
Ikiwa ni fedha za awali za utekelezaji wa miradi mkakati na kati ya fedha hizi kiasi cha Shs. 400,000,000 kimewekezwa kwenye mfuko wa dhamana wa SAMIA BOND. Wakati mchakato wa utekelezaji wa miradi mingine ukiwa unaendelea.
Picha: Baadhi ya wajumbe wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika
wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani.
"Katika kuongeza tija ya shughuli za kilimo ili kuboresha maisha ya Wananchi wa Wilaya ya Tanganyika, Halmashauri imeweza kufanya Usajili wa wakulima 30 kila kijiji na usajili wa mashamba yao, kuchukua taarifa za awali (base information), kutoa Elimu ya uzalishaji wa mahindi kwa tija, kuchukua sampuli za udongo(jumla ya sampuli 389 zimechukuliwa) katika mashamba ya wakulima wote 240 yaani 30," amesema Luziga.
Kwa upande wake afisa tawala msaidizi uchumi na uzalishaji Nehemia James akizungumza na madiwani wa Halmashauri hiyo amewashauri kuwekeza katika miradi ambayo itatua changamoto za wananchi kama vile changamoto za ufugaji kwa kuanzisha ufugaji wa kisasa wa ngombe wa maziwa kutokana na kuwa wilaya hiyo inaongoza kwenye ufugaji.
Mwisho.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi
Telephone: 025-2957108
Mobile:
Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.