• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

Posted on: May 28th, 2025

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Profesa Ibrahim Juma, ameongoza kikao muhimu kati ya Watumishi wa Mahakama na Wadau wa Mahakama mkoani Katavi, ambapo amesisitiza uadilifu miongoni mwa watendaji wa Mahakama pamoja na mchango wa wadau katika kuimarisha huduma za utoaji haki nchini.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Mei 28, 2025 katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Profesa Juma amesema kuwa uadilifu kwa watumishi wa Mahakama ni nguzo kuu ya kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wakati, kwa usawa na bila upendeleo. Ameeleza kuwa Mahakama haiwezi kutimiza wajibu wake ipasavyo pasipo misingi imara ya maadili, weledi na uwajibikaji.

Aidha, Jaji Mkuu amesisitiza umuhimu wa ushirikiano kutoka kwa taasisi mbalimbali za umma katika kutekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2050. Amebainisha kuwa mafanikio ya dira hiyo yanahitaji mshikamano wa kitaifa pamoja na kujenga mfumo wa haki unaoendana na mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kiteknolojia.

Kwa upande wake, Jaji Kiongozi na Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. Mustapher Siyani, amewasihi viongozi wa umma na wananchi kwa ujumla kuepuka kujadili mashauri yanayoendelea mahakamani, akieleza kuwa hali hiyo huathiri mwenendo wa kesi na hupunguza imani ya wananchi kwa mfumo wa utoaji haki

Mhe. Siyani pia amewahamasisha wananchi wa Katavi kuchangamkia fursa za ajira kama madalali na wasambaza nyaraka wa Mahakama, akibainisha kuwa kwa sasa mkoa wa Katavi una dalali mmoja pekee kati ya 118 waliopo nchi nzima.


Akihitimisha kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, amemshukuru Jaji Mkuu kwa kufanya ziara hiyo mkoani Katavi na ameahidi ushirikiano wa karibu na Mahakama katika kuhakikisha haki inatolewa kwa mujibu wa sheria na inawafikia wananchi wote.

RC Mrindoko ameahidi kuwa Katavi itakuwa kinara wa ujenzi wa maboma ya Mahakama, na ameukaribisha uongozi wa Mahakama kufanya shughuli za kitaifa na kikanda mkoani Katavi, akitaja vivutio vya mbuga ya Katavi, misitu ya asili na fursa ya biashara ya kaboni kama sehemu ya utajiri wa mkoa.


Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • RC MRINDOKO AKEMEA WAKURUGENZI KUZALISHA MADENI MAPYA KWA WAZABUNI.

    May 22, 2025
  • KATAVI YAFUNGUA MILANGO YA UWEKEZAJI.

    May 21, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.