• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

HALI YA LISHE

Posted on: September 12th, 2017

WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI WATAKIWA KUZINGATIA MASUALA YA LISHE

Bi.Asnath Mrema Afisa Lishe Mkoa wa Katavi akiongea na walengwa wa Mpango wa TASAF Mkoa wa Katavi amesema kuwa Mkoa wa Katavi bado haufanyi vizuri sana katika suala zima la lishe, hali ambayo inachangia kuwa na athari nyingi zinazotokana na hali ya lishe moja kwa moja au zinazochangia kuwepo na matatizo mengine ya kiafya kwa jamii ya wanakatavi kwa ujumla wake.

Bi.Asnath amesema kuwa pamoja na kuwa Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha chakula kwa wingi bado Mkoa unakabiliwa na tatizo kubwa la lishe kwa wananchi wake. Lishe duni ni moja ya matatizo makubwa ya kiafya yanayoathiri haswa watoto wadogo, wachanga na wanawake walio katika umri wa kuzaa nchini. Kwa watoto chini ya miaka 5 tafiti zinaonyesha kuwa hali ya udumavu katika Mkoa wa Katavi ni asilimia 39 ukilinganisha na asilimia 34 kitaifa. Uzito pungufu ni asilimia 15.4 kwa Mkoa wa Katavi na kitaifa ni asilimia 14.0. Upungufu wa damu  ni asilimia 54.9 kimkoa na Kitaifa  ni asilimia 57. Bi.Asnath amesema kuwa moja ya changamoto  inayowakabili wanawake wenye umri wa miaka 15 – 49 ni upungufu wa damu ambapo kati ya wanawake kumi (10) watano (5) wanaupungufu wa damu.        

Bi.Asnath amewaeleza walengwa hao kuwa pamoja na changamoto hizo Mkoa wa Katavi umejiwekea mikakati mingi ikiwemo, Kuhakikisha shughuli za lishe zimepangwa katika mipango ya idara mbalimbali ambazo zinahusika na masuala ya lishe kama Afya, Elimu, Kilimo, maendeleo ya jamii na maji. Kuendelea kutoa chanjo kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka 5 na matone ya vitamin ‘A’ na dawa za minyoo kwa akinamama wajawazito na watoto chini ya miaka 5. Kuhimiza kila mkazi wa eneo la halmashauri mwenye uwezo wa kufanya kazi kuwa na shamba kwa ajili ya kuzalisha mazao ya chakula, mazao ya biashara, mbogamboga na matunda kwa ajili ya kupunguza tatizo la upungufu wa chakula na umasikini wa kipato ngazi ya kaya. Kuhusu suala la usalama wa chakula Bi.Asnath amesema kuwa imezuka tabia ya wakulima kuuza mazao yao yakiwa shambani, hii ni hatari na jambo ambalo linatakiwa kukemewa kwa nguvu zote na kuwataka walengwa waliopo katika Mpango wa TASAF kuhakiksha kuwa wanahifadhi chakula.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • RC MRINDOKO AZINDUA MSIMU WA UNUNUZI WA PAMBA NA MAZAO MENGINE KWA MWAKA 2025/26

    June 09, 2025
  • RC MRINDOKO AKUTANA NA WAENDESHA BODABODA KATAVI, ATOA WITO WA AMANI NA USHIRIKI UCHAGUZI MKUU 2025.

    June 05, 2025
  • JAJI MKUU WA TANZANIA ASISITIZA UADILIFU NA USHIRIKIANO WA WADAU KATIKA UTOAJI HAKI.

    May 28, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.