• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA MADAWATI SHULE YA WASICHANA KATAVI

Posted on: August 12th, 2025

Benki ya CRDB Mkoa wa Katavi imetoa madawati 60 kwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Katavi, iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo, ikiwa ni sehemu ya mpango wa benki hiyo wa kurudisha fadhila kwa wananchi kupitia faida iliyopatikana.

Akikabidhi madawati hayo, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Bi Jennifer Tondi, ameeleza kuwa Benki ya CRDB kupitia mkakati wake wa Keti Jifunze itaendelea kushirikiana na serikali katika kuchangia huduma mbalimbali za kijamii mkoani Katavi.

Amesema kuwa pamoja na majukumu yake ya kibenki, benki hiyo imetenga asilimia moja ya faida yake ili kuhudumia mahitaji ya jamii katika sekta mbalimbali, ikiwemo elimu.

Aidha, ameeleza kuwa lengo ni kuhakikisha tatizo la wanafunzi kuketi chini linaondolewa kabisa kupitia kampeni ya Keti Jifunze, na kwamba benki itaendelea kushughulikia changamoto ya upungufu wa madawati mashuleni kadri faida itakavyopatikana.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Mhe. Jamila Yusuph, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi, ameishukuru Benki ya CRDB kwa mchango wake katika maendeleo ya wilaya hiyo, amewataka wadau wengine kuendelea kujitokeza kuchangia maendeleo, na amewasisitiza wanafunzi kusoma kwa bidii pamoja na kuyatunza madawati hayo ili yaweze kusaidia vizazi vijavyo.

Aidha, ametoa wito kwa wanafunzi hao kuepuka mahusiano ya kimapenzi katika kipindi cha masomo yao, akisisitiza kuwa kufanya hivyo kutawawezesha kuzingatia elimu na kujiepusha na changamoto zinazoweza kuhatarisha maisha yao ya baadaye.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • RATIBA YA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI - MWAKA 2025 April 28, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA KATAVI August 27, 2025
  • TAARIFA YA MAENDELEO YA SEKTA YA VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI MKOA WA KATAVI August 27, 2025
  • View All

Latest News

  • RC MRINDOKO AKAGUA MIRADI YA MAJI MPANDA, ATOA MAAGIZO YA KUONGEZA KASI YA UTEKELEZAJI.

    September 03, 2025
  • RC MRINDOKO AHIMIZA AMANI NA USHIRIKIANO KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025.

    September 01, 2025
  • MFUMO WA E - MABORESHO KUIMARISHA UTENDAJI KWA WATUMISHI WA UMMA.

    August 26, 2025
  • MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA YAFIKIA TAMATI, DC BUSWELU AWASISITIZA UZALENDO

    August 26, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.