• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Katavi Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
  • Services
  • Administration
    • Departments
      • Adm and HR
      • Planning and Coordination
      • LGA.s
      • Infrustructures
      • EPSS
      • Water
      • Healthy
      • Education
    • Units
      • Information and Communication Technology
      • Finance and Accounts
      • Procurement and Management
      • Legal
      • Internal Auditor
    • Organization Structure
  • Publications
    • Guidelines
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events
  • Projects
    • Completed projects
    • On Going Projects
  • Districts
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Investment Opportunities
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Tourism
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

Bandari Karema yaanza Kazi.

Posted on: September 1st, 2022

Pichani:Moja kati ya Boti za Kitalii ilipotia nanga katika Bandari ya Karema mara baada ya Bandari hiyo kuanza kutumika 1 Septemba 2022.

Tanganyika -Katavi 

Wananchi na Wafanya biashara wasafirishaji wa bidhaa katika Mwambao wa ziwa Tanganyika wametakiwa kuachana na Bandari zisizo rasmi na badala yake kutumia Fursa ya Bandari ya kisasa ya Karema iliyoanza kutumika 1 Septemba 2022 kwa shughuli za kusafiri na Usafirishaji wa Bidhaa zao.

Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Onesmo Buswelu amemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko ambapo 1 Septemba 2022 amefika katika Bandari ya Karema kushuhudia kuanza kwa shughuli za usafirishaji  Bandarini hapo.

Akizungumza  na Baadhi ya Wananchi Bandarini hapo DC Buswelu amewataka Wananchi na Wafanyabiashara wanaofanya shughuli za Usafirishaji katika mwambao wa Ziwa Tanganyika pamoja na Wananchi watakaosafiri kupitia Bandari mpya kutunza Miundombinu ya Bandari hiyo kusudi iweze kutoa huduma kwa muda mrefu zaidi.

Mhe.Buswelu ameitaka Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA pamoja na Shirika la Uwakala wa Meli Nchini TASAC kushawishi Meli  kubwa kutoka Kongo na Maeneo mengine kutia nanga katika Bandari ya Karema.

Shabani Juma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganganyika amemshukuru Rais Samia kwa Ujenzi wa Bandari hiyo ambapo ametoa rai kwa Wafanyabiashara wanaosafiri kwenda Kongo kutoka Dar es slaam na Maeneo mengine Nchini kutumia Barabara ya Tabora Mpanda iliyo katika kiwango cha Lami kurahisisha kufika kwa urahisi katika Badari ya Karema.

Naye Diwani wa Kata ya Karema Bw. Michael Kapata pamoja na shukrani alizozitoa  kwa Serikali amesisitiza juu ya umuhimu wa Ujenzi wa Barabara kwa kiwango cha Lami kutoka Mpanda Karema ili kurahisisha shughuli za Uchukuzi na Usafirishaji wa Bidhaa kutoka Mpanda Mjini hadi Karema Bandarini.

Kaimu Meneja Mfawidhi wa bandari za TPA Ziwa Tanganyika Edward Mabula ameeleza kuwa Zaidi ya boti 4 za Abiria pamoja na Boti za Utalii zimewasili Bandarini hapo ambapo abiria 35 wamepokelewa katika Bandari hiyo wakitokea maeneo mbalimbali ya mwambao wa Ziwa Tanganyika.

Bandari hiyo iliyogharimu Bilioni 47.9 ilihusisha ujenzi wa kivunja mawimbi, mlango bandari na gati ya meta 150 zenye uwezo wa kulaza meli zenye urefu wa meta 75 na upana wa meta 15, uchimbaji na uwekaji wa kina wa mlango wa bandari, jengo la ofisi, sebule ya abiria na shehena ya jumla.

Announcements

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • View All

Latest News

  • BARAZA MAALUM LA MADIWANI TANGANYIKA LAJADILI TAARIFA YA CAG, WATUMISHI WATAKIWA KUFUATA SHERIA.

    June 17, 2025
  • RAS MSOVELA AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO KWA KUTEKELEZA MAAGIZO YA KAMATI YA BUNGE.

    June 19, 2025
  • MAADHIMISHO SIKU YA MTOTO AFRIKA, CHAGULAGA BADO NI KILIO KWA WASICHANA KATAVI.

    June 16, 2025
  • RC MRINDOKO ATOA WITO KWA VIONGOZI KUHAMASISHA MATUMIZI YA CHAKULA CHENYE VIRUTUBISHI ILI KUTOKOMEZA UDUMAVU.

    June 10, 2025
  • View All

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
More Videos

Quick Links

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Related Links

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Location Map

Contact Us

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Postal Address: Box 235, Mpanda -Katavi

    Telephone: 025-2957108

    Mobile:

    Email: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2017 Katavi RS . All rights reserved.