Mradi wa Ujenzi wa Zahanati ya Kikonko iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ni moja ya miradi ya miundombinu ambayo inatekelezwa na Mpango wa TASAF awamu ya tatu. Miradi mingine ya ujenzi inayotekelezwa na TASAF awamu ya tatu katika Mkoa wa Katavi ni Ujenzi wa Zahanati ya Mlima Kipara katika kijiji cha Mwamkulu Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda na Ujenzi wa Zahanati ya Itetemnya ambayo ipo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Ujenzi wa Zahanati ya Kikonko umekamilika ambapo jumla ya Shilingi 82,617,912.00 zimetumika, kati ya hizo shilingi 74,694,600.00 zimetolewa na TASAF na shilingi 8,667,000.00 ni mchango wa wananchi. Lengo la miradi hii ni kusogeza huduma za Afya kwa jamii hasa kwa vijiji ambavyo havina huduma hizo.
Zahanati ya Kikonko katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved