Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi, kama ilivyoelekezwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa (MB) wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi Mkoani Katavi tarehe 25 hadi 27 Agosti 2021. Utaratibu wa namna pande zote mbili zinavyoshiriki katika ujenzi wa Hospitali hiyo umeanishwa vyema katika Hati ya Makubaliano (MoU) ambayo imesainiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Katika Hati ya Makubaliano (MoU) iliyosainiwa jukumu kubwa la Katibu Mkuu-Afya ni kuandaa bajeti na kufuatilia upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kuendeleza ujenzi pamoja na kuingia mikataba yote ya ujenzi. Kwa upande wa Katibu Tawala Mkoa jukumu kubwa ni kusimamia matumizi ya fedha za ujenzi kwa kuratibu na kusimamia manunuzi ya vifaa vya ujenzi, malipo ya Mkandrasi na Malipo ya Mshauri Elekezi kupitia kamati alizoziunda kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu pamoja na kusimamia na kufuatilia shughuli za ujenzi zinazoendelea kila siku.
Ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi unatekelezwa kwa awamu kama ifuatavyo kulingana na upatikanaji wa fedha, awamu ya kwanza ya ujenzi wa mradi huu ilianza na majengo matatu ambayo ni Jengo kuu lenye ghorofa moja lenye Kitalu A na B litakalotoa huduma za afya ya uzazi mama na mtoto (Maternity), huduma za dharura (EMD), wagonjwa wa Nje (OPD), Famasi, huduma za Radiolojia, Huduma za upasuaji na huduma za uangalizi Maalumu (ICU) pamoja na jengo la Maabara.
Utekelezaji wa ujenzi huu ulianza mwezi Mei, 2018 chini ya usimamizi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambapo ulikuwa utekelezwe kwa kipindi cha wiki 48 kwa gharama ya Tsh.9.7b. Aidha ilipofika Februari 2019, mradi ulikabidhiwa Wizara ya Afya ukiwa kwenye hatua ya msingi sawa na asilimia 20 ukiendelea kutekelezwa na Mkandarasi SUMA JKT kwa mfumo wa Kandarasi (conventional method). Mradi huu uliendelea kutekelezwa kwa utaratibu wa kandarasi mpaka mwezi April 2021 ukiwa katika asilimia 43 ya utekelezaji ambapo Tsh.3.6b zilitumika. Serikali iliamua kubadilisha mfumo wa utekelezaji wa mradi huu kwenda kwenye mfumo wa “Force account” ili kuharakisha utekelezaji wa mradi huu.
ili kufanikisha utekelezaji wa mradi huu kwa utaratibu wa “Force Account”, Serikali kupitia Wizara ya Afya ilikamilisha taratibu za manunuzi za kumpata Mshauri elekezi na Fundi mjenzi ambapo Mshauri Elekezi ni Crystal consultant na Fundi mjenzi ni SUMA JKT, kwa sasa gharama za kukamilisha mradi huu zinakadiriwa kuwa Tsh.12b ambapo 1.98b ni gharama za ufundi atakazolipwa SUMA JKT na kiasi cha Tsh.10.2b kitatumika kumlipa Mshauri Elekezi na kununua vifaa vya ujenzi.
Mkandarasi alikabidhiwa site tarehe 15 Septemba 2021 kwa ajili ya kuanza shughuli za ujenzi na mradi ulipaswa kukamilika tarehe 14/11/2022, hata hivyo ujenzi haukuanza katika muda huo kutokana na changamoto za ucheleweshaji wa kibali cha matumizi ya fedha za ujenzi na taratibu za manunuzi ambapo zilipotea siku 58. Muda wa ujenzi uliopangwa ni miezi 10, aidha mpaka sasa Serikali imeshatoa kiasi Jumla ya Tsh bilioni 9.28 kwa ajili ya kundeleza ujenzi , kwa sasa ujenzi unaendelea na uko katika hatua ya umaliziaji (ufungaji wa CT scan, ufungaji wa LIFT na ufungaji wa mifumo ya gesi tiba) Pamoja na kazi za nje, kiujumla utekelezaji wa mradi umefikia 98% kwa upande wa Wing A. Hata hivyo Hospitali tayari imeshaanza kufanya kazi, kazi zilizobakia zinaendelea kushughulikiwa wakati huduma zikiendelea kutolewa.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved