Akizeti ni miongoni mwa mazao yanayolimwa mkoani Katavi kwa ajili uzalishaji wa mafuta ya kula. Tanzania haijajitosheleza katika uzalishaji wa mafuta ya kula. Tanzania huagiza zaidi ya 60% ya mafuta ya kula kutoka nje kwa ajili ya matumizi ya ndani ya nchi. Hela nyingi sana zinatoka nje ya nchi badala ya kuzunguka ndani ya soko la Tanzania. Serikali imejipanga kuondoa tatizo kwa kuhamasisha wananchi kulima mazao yatakayozalisha kwa wingi mafuta ya kula nchini. Kwa muktadha huo, Kiongozi mkuu katika serikali ya Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko anajitokeza kwa wananchi kuwahamassha kuzalisha mafuta kwa wingi mafuta ya alizeti ili kuondoa uhaba wa mafuta katika mkoa wake.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved