Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amewataka wakurugenzi wa halmashauri zake kubuni vyanzo vipya vya mapato ili kujenga uwezo mkubwa zaidi wa serikali katika utoaji wa huduma zake kwa wananchi.
Mhe. Mrindoko amesema hayo wakati akifungua kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wa katavi katika ukumbi wa Manispaa Mpanda mjini Mpanda huku akiziasa halmashauri hizo kuachana na ukusanyaji mapato wa kimazoea ili kupata mapato ya kutosha.
Amesema tumezoea kila mwaka kukusanya mapato ya fedha za ndani kutokana na ushuru wa mazao, ushuru wa misitu, ushuru wa masoko na kuhoji hivi ikitokea kwamba tumekosa mapato kutoka vyanzo hivyo, je tutapata wapi fedha ya kuendesha shughuli za serikali?
Mhe. Mrindoko amesema kama mkoa tunapaswa kubadilika na kuibua vyanzo vingi vya mapato ili kupanua wigo wa mapato ya serikali utakaoweza kuhimili utekelezaji wa miradi mbali mbali kwa wananchi
Hadi kufikia Januari 2023, mkoa wa katavi umekusanya bili 9.4 kati ya lengo la bil. 14 ambalo kama mkoa imeliweka kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Amewapongeza wakurugenzi kwa kufikia na kuvuka lengo walilojiwekea katika makusanyo ya mapato ya mwaka wa fedha /20222023.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved