Zaidi ya wanahabari 20 kutoka katika Wilaya na Halmashauri mbalimbali za Mkoa wa Katavi wamepatiwa mafunzo ya Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini TASAF yaliyoratbiiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Kichangani Lodge ulioko Manispaa ya Mpanda yamewakutanisha Maafisa Habari Mawasiliano na Uhusiano,Waratibu wa TASAF Halmashauri na Mkoa pamoja na Waandishi wa Habari kutoka katika Vyombo mbalimbali vya Habari mkoni Katavi
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TASAF Makao makuu Bi.Zuhura Mdungi amesema mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari, na Maafisa Habari kuwa na uelewa wa namna ambavyo Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini TASAF unatekeleza shughuli zake mbalimbali kupitia Programu mbalimbali zinazotekelezwa na Wadau Wakiwemo Halmashauri,pamoja na Mikoa
Amesema Wanahabari ni wadau muhimu katika kutangaza shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na TASAF hivyo wanapaswa kushirikishwa katika shughuli mbalimbali zinahohusu TASAF kwa lengo la kusaidia kuutangaza mpango huo.
Aidha amesisitiza kuwa wanahabari wanayo nafasi kubwa katika jamii kwa kuwa ni waelimishaji wa wakubwa katika mambo mbalimbali hivyo ni jukumu lao pia kuijengea jamii uelewa wa namna ambavyo TAFAF inatekeleza program mbalimbali kwa manufaa ya Wananchi
Akizungumzia baadhi ya changamoto zilizokuwa zikijitokeza katika suala la kuandika na kutangaza mpango wa TASAF,Bi.Mdungi amesema awali baadhi ya waandishi hawakuwa na uelewa wa namna ambavyo TASAF inatekeleza shughuli zake mbalimbali jamo ambalo lilipelekea jamii kutokuwa na uelewa kuhusu TASAF.
Hata hivyo Bi.Mdungi amebainisha kuwa kwa sasa TASAF Inaendelea kuboresha mazingira kwa wanahabari sambamba na kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari ,Maafisa Habari pamoja na Wadau mbalimbali katika kuhakikisha kuwa kupitia Vyombo vya Habari jamii inakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu malengo mahsusi ya Mpango wa TASAF.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved