Mazingira ni nyumba yetu tunapoishi na kufanya shughuli mbali mbali za ustawi na maendeleo yetu sisi wanadamu. Tunapenda kuona nyumba safi na yenye mandhari safi. Hata hivyo ukiangalia katika mazingira yetu utaona kwamba tumeyaharibu kutokana na tabia zetu wenyewe ambazo zinaathiri na zinaendelea kuathiri mazingira yetu kiasi ambacho inatishia uhai na maisha yetu. Hatuwezi kuendelea kuona na kushangilia mazingira yetu yanavyoendelea kuharibika kwa sababu mazingira ni maisha na uhai wetu sasa na baadaye, lazima kama jamii tuchukue hatua za kusafisha mazingira yetu kwa ajili ya afya bora,ustawi wetu na maendeleo ya sasa na yajao. Sasa katika kuhakikisha kuwa mazingira yetu yapo safi na yanaendelea kuwa safi na kutusaidia sisi wanadamu, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Jamillah Yiusuf, anajitokeza hadharani kuzindua Mkakati wa Usafi na Utunzaji wa Mazingira katika Mkoa wa Katavi, katika eneo la Mpanda Hotel, 23/4/2022 mjni Mpanda ili kuhamasisha wananchi kufanya usafi na kutunza mazingira yetu kwa ustawi wa sasa na baadaye
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved