Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimefanikisha utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa majengo mapya katika Kampasi ya Mizengo Pinda, Katavi, kupitia mradi wa HEET. Hafla hiyo imehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe.Mwanamvua Mrindoko kama mgeni rasmi.
Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa SUA, Prof. Raphael Chibunda, mradi huo utagharimu takribani TZS Bilioni 17. Ujenzi huo unahusisha jengo lenye madarasa, ofisi, na bweni la wanafunzi.
Kupitia mradi huo, SUA itaongeza uwezo wa kudahili wanafunzi na hivyo kuwapa fursa zaidi vijana wa Kitanzania kupata elimu ya juu.
Mradi wa HEET (Higher Education for Economic Transformation) ni mpango mkubwa unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Benki ya Dunia. Lengo kuu la mradi huu ni kuimarisha na kuboresha mifumo ya elimu ya juu nchini ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved