• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

SERIKALI YANUIA KUWALINDA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI

Posted on: July 10th, 2025


Kuelekea uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, serikali imeweka mikakati Thabiti ya kuhakikisha kuwa katika  kipindi  cha uchaguzi kila mwanahabari anakuwa salama yeye pamoja na vifaa vyake kupitia jeshi la polisi ili waweze kufanya kazi katika mazingira salama, Rafiki na yenye uhuru wakati wakitekeleza majukumu yao.

Mikakati hiyo imetolewa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025, Julai 9, 2025 jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambapo amewaasa waandishi wa habari nchini kuwa walinzi wa ukweli, wajenzi wa amani na kuchochezi wa uwajibikaji wa kisiasa.

PICHA; Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025.

Ameeleza kuwa Katika kipindi hiki cha uchaguzi wandishi wa habari wanapaswa kuwa walezi wa maudhui ya habari yanayokwenda kwa jamii, mjue kuwa katika habari hizo taifa litabaki moja aidha limegawanyika, hivyo wanawajibu wa kuwa walinzi wa kweli na wajenzi wa amani huku wakiwabaini wachochezi katika tasnia ya habari na kuwawajibisha bila kusubiri vyombo vya dola.

Amevitaka vyombo vya habari kuwa kioo cha jamii na kujiepusha na uzushi, chuki au upendeleo na badala yake kuhimiza maelewano, uvumilivu wa kisiasa, na utamaduni wa kuheshimu tofauti za maoni.

"Ni wajibu wa Serikali kuhakikisha waandishi wa habari katika kipindi chote cha mchakato wa uchaguzi wanabaki salama pamoja na vitendea kazi vyao. Aidha, Serikali, tutaendelea kulisimamia hili kwa nguvu zetu zote. Tutahakikisha kuwa, mnakuwa na mazingira salama, huru na rafiki wakati wote wa majukumu yenu,". amesema Dkt. Biteko

.

PICHA; Baadhi ya wajumbe waliohudhuria wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025.

Ameendelea kusema kuwa  kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 katika jamii kutakuwa na watu wenye mitazamo tofauti kulingana na vipaumbele vyao hata hivyo vyombo vya habari vina fursa ya kutoa uelekeo kwa taifa.

"Uchaguzi ni kipindi cha muda mfupi, tumuombe Mungu hata baada ya Uchaguzi tubaki kuwa Taifa moja lenye ustahimilivu na kila mmoja akitoka kwake aende kutafuta mkate arudi nyumbani kwa familia yake kukiwa na amani, sisi kupitia mkutano huu tuungane kuhakikisha Taifa letu linabaki salama. Sekta ya habari ni nyenzo muhimu katika kulinda na kudumisha amani katika kipindi chote cha uchaguzi," amesisitiza Dkt. Biteko.

PICHA; Baadhi ya wajumbe waliohudhuria wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wadau Kujadili Mchango wa Sekta ya Habari katika kufanikisha Uchaguzi Mkuu 2025.

Kutokana na mazingira wezeshi kwa sekta ya habari nchini  idadi kubwa ya vyombo vya habari imeongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita, ambapo kuna jumla ya magazeti 375, vituo vya redio 247, vyombo vya habari vya mtandaoni 355, blogs 72 na vituo vya televisheni 68.

MWISHO.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HUDUMA YA KUCHUJA DAMU (DIALYSIS): TUMAINI JIPYA KWA WAGONJWA WA FIGO KATAVI.

    July 21, 2025
  • VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUTUMIA MADHABAHU KUKEMEA NA KUELIMISHA UMMA JUU YA MADHARA YA RUSHWA KATIKA UCHAGUZI.

    July 18, 2025
  • BEVAC YAWEKA MSUKUMO MPYA KWENYE SEKTA YA UFUGAJI NYUKI NSIMBO.

    July 10, 2025
  • SERIKALI YANUIA KUWALINDA WAANDISHI WA HABARI KATIKA KIPINDI CHA UCHAGUZI

    July 10, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved