SERIKALI MKOA WA KATAVI KUPANDISHA MADARAJA WATUMISHI 823
Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi Bw. Hassan Rugwa amesema ofisi yake inatarajia kupandisha madaraja watumishi 823 katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Bw. Rugwa amesema hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashaulili Mjini Mpanda
Amesema amepokea maelekezo ya kupandisha watumishi madaraja kutoka serikali kuu na kuongeza kuwa tayari kibali cha kupandisha watumishi hao wameshapata na mchakato wa utekelezaji huo umeshapelekwa kwenye mamlaka zinazohusika kwa ajili ya utekelezaji zoezi hilo.
Bw. Rugwa amewapongeza watumishi wote wa mkoa wake kwa ufanisi waliopata katika utekelezaji wa majukumu yao kwa wananchi licha ya kukabiliwa na changamoto mbali mbali katika utumishi wao.
Amebainisha baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na uhaba wa watumishi unaoukabili Mkoa wa Katavi. Hata hivyo, kwa kutambua changamoto hizo serikali kuu imeendelea kukabiliana na upungufu huo.
Bw. Rugwa amesema kuwa tayari serikali imeshaajiri watumishi 316 ambao mkoa umeshwapokea na kuwapeleka katika idara na halmashauri za mkoa wake.
Amewapongeza wafanyakazi wa Mkoa wa Katavi kwa kazi nzuri walizozifanya, kwa umoja na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao na kuwasihi kuendelea kudumisha umoja, mshikamano na uzalendo katika utekelezaji wa kazi zao
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved