Mkoa wa Katavi umeanda tamasha kubwa la Samia Day ili kutangaza Mafanikio ya Serikali yaliyopatikana kwa kipindi cha miaka 5 ya Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika kuanzia Juni 4, hadi 05, 2025 katika Viwanja vya Shule ya Msingi Inyonga vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ambapo mgeni Rasmi atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwanamvua Hoza Mrindoko.
PICHA: Katibu tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela akizingumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutambulisha Tamasha la Samia Day.
Akizungumza na waandishi wa habari Katibu tawala mkoa wa Katavi Albert Msovela leo Juni amesema kuwa lengo ni Kumpongeza na kumshukuru Mheshimiwa Rais kwa mchango wake wa kuleta fedha Zaidi ya Trilioni 1.3 ambazo zimesaidia kutekelezwa kwa miradi mingi ya maendeleo Mkoani Katavi katika Sekta zote za maendeleo na huduma kwa Jamii.
“Kauli mbiu katika inayobeba tamasha hilo “Asante Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa fedha za Maendeleo, Katavi Imara na Maendeleo Imara” likihusisha Serikali ya Mkoa wa Katavi, Taasisi zote na kwa kushirikiana na timu kizimkazi maarufu kama Mkasi Utaongea,”. Amesema Msovela.
Amesema kuwa Juni 04,2025 TIMU KIZIMKAZI (Mkasi Utaongea), Viongozi na Wataalam watapata fursa ya kutembelea Hifadhi ya Katavi pamoja na kujionea uzuri wa asili wa mbuga ya Katavi national park, Kuona miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Mradi wa Maji wa Miji 28 uliopo Shanwe, Vihenge vya kuhifadhia mazao, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na kituo cha kupozea umeme wa Grid ya Taifa.
Aidha Kutakuwa na Usiku wa Mama Samia tukio litakalofanyika katika ukumbi wa Mpanda Social Hall ambapo baadhi ya Viongozi watapata fursa ya kuongea na kubadilishana mawazo kuhusu Mkoa tulipotoka, tulipo kwa sasa na tunakoelekea.
PICHA: Katibu tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela akizingumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutambulisha Tamasha la Samia Day.
Msovera ameongeza kuwa Tarehe Juni 5, 2025 itakuwa kilele cha Samia Day ambapo yataanza Matembezi ya hiari kuanzia Saa 01:30 asubuhi ambayo yatafanyika katika Mji wa Inyonga Wilayani Mlele ambayo yataongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mheshimiwa Mwanamvua Hoza Mrindoko.
“Michezo itakayofanyika itajumuisha Mpira wa Miguu, Kuvuta Kamba, Kukimbia na Magunia, Kufukuza kuku na Mbio za mita 100 hivvyo tunawaomba Wananachi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika tukio hilo muhimu na la kihistoria katika Mkoa wetu.
PICHA: Katibu tawala Mkoa wa Katavi Albert Msovela akizingumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kutambulisha Tamasha la Samia Day.
Ameongeza kwa makundi yote katika Jamii wakiwemo Bodaboda, Wasanii, Bajaji, Mama Lishe, Machinga na makundi mengine kujitokeza kwa wingi katika Matembezi ya Hiari na maadhimisho yote kwa ujumla. Vilevile, Taasisi zote za Serikali na zisizo za Serikali, Mashirika ya Kiraia, Sekta binafsi na Wadau wa maendeleo kujumuika pamoja katika siku hiyo.
Mwisho.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved