Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amezindua shughuli ya ugawaji wa vitambulisho vya kieletroniki kwa wajasiriamali na wafanyabiashara ndogodogo vinavyotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum.
Uzinduzi huo umefanyika Desemba 03, 2024 wakati wa kikao cha pili cha Baraza la biashara la Mkoa.
Akizungumza wakati shughuli hiyo, Mheshimiwa Sawala amewahamasisha wafanyabiashara ndogondogo mkoani humo kujisajili ili kupata Vitambulisho hivyo ambavyo vitawasaidia kupata fursa mbalimbali zitakazo kuuza biashara zao ikiwemo mikopo yenye riba nafuu iliyotengwa na Serikali.
Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Katavi, Anna Shumbi ameeleza sifa za wanaotakiwa kupatiwa vitambulisho hivyo kuwa ni lazima mfanyabiashara awe na biashara ndogo ndogo.Akieleza utofauti uliopo kati ya vitambulisho vya sasa na vile vilivyokuwa vikitolewa awali, Anna amesema kitambulisho cha sasa ni cha kisasa zaidi ambapo taarifa za mhusika zinaingiliana na mamlaka mbalimbali za kiserikali ikiwemo Kitambulisho cha Taifa (NIDA), Benki na Mamlaka zingine.Lengo kuu la vitambulisho hivyo ni kuwatambulisha wafanyabiashar kwenye taasisi mbalimbali.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved