Wenyeviti na Wajumbe wa Serikali ya Mtaa, Vijiji na Vitongoji katika mkoa wa Katavi wameapishwa Novemba 29/2024 tayari kuanza kutekeleza majumu yao ya kazi.
Akizungumza baada ya viongozi hao kula kiapo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amewaasa Viongozi hao kwenda kuwatumikia Wananchi ipasavyo bila kujali itikadi za vyama vyao vya siasa.
Rc. Mrindoko ameongeza kuwa Viongozi hao wanapaswa kuweka mikakati thabiti inayotekelezeka itakayoleta tija kwa maendeleo ya jamii.
Pamoja na hayo Rc. Mrindoko ameendelea kuwahimiza Viongozi hao kutekeleza 4R katika utendaji kazi wao pamoja na kufuata sheria,kanuni na miongozo mbalimbali inayotolewa na Serikali.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved