Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, leo Januari 1, 2025, amekabidhi msaada katika Gereza la Mahabusu Mpanda kama sehemu ya kutoa salamu za mwaka mpya kwa wahitaji kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema kuwa jamii inapaswa kutambua kwamba wafungwa ni raia na kifungo ni sehemu ya mafunzo, si laana kama inavyotafsiriwa. Amelishukuru na kulipongeza pia Jeshi la Magereza kwa kazi kubwa wanayoifanya, ikiwemo utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoleta mafunzo kwa wafungwa ili watakapomaliza kifungo waweze kuwa raia wema wenye ujuzi na uwezo wa kufanya kazi.
Pia, Rc Mrindoko ametumka nafasi hiyo kuwaombea heri ya mwaka mpya wafungwa, akisema kwamba uwe mwaka mzuri na Mwenyezi Mungu awaonyeshe haki yao wanayostahili.
Naye Mkuu wa Gereza la Mahabusu Mpanda, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza Frank Mwakatobe, amemshukuru Mkuu wa mkoa kwa kufanya ziara ya kutembelea gereza hilo.
"Kuna makundi mengi yenye uhitaji wa msaada kama tulivyoupata leo, lakini Mkuu wa Mkoa ameona ni vyema kuhusika katika urekebishaji. Tunamshukuru sana na wafungwa wa mahabusu wamefurahi na wanamshukuru kwa zawadi hizi." Amesema Mwakatobe.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved