Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akipokea maelezo kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Bwala la Maji Nsenkwa kutoka kwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mlele Bw.Gilbert Isack wakati alipofanya ziara kukagua Mradi huo wa Maji.
Mlele -Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amemuomba Waziri wa Maji pamoja na RUWASA Makao makuu kusaidia kutatua changamoto zinazosababisha kusua sua kwa ujenzi wa Bwala la Maji Nsenkwa lililopo katika Kijiji cha Nsenkwa Kata ya Nsenkwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele ili Wananchi waondokane na changamoto ya Uhaba wa Maji.
Ujenzi wa Bwawa hilo la Maji linalotegemewa kuondoa adha ya Maji kwa Wakazi wa takribani Vijiji 16 katika Wilaya ya Mlele umeendelea kusuasua kumalizika kwa takribani miaka 4 ikiwa ni tangu kuanza utekelezaji wake Mwaka 2018.
Akizungumza wakati wa Ziara yake 27 Agosti 2022 kukagua mradi huo wa Maji Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema licha ya changamoto ya mawasiliano iliyowasilishwa na uongozi wa RUWASA ngazi ya Wilaya katika Taarifa yake kuhusu utekelezaji wa mradi huo bado kuna changamoto ya Mkandarasi kutokuwa makini katika utekelezaji wa mradi huo.
“Nimeona hapa kuna matatizo ya aina mbili la kwanza ni kwa Mkandarasi Mwenyewe yaani spidi yake sio nzuri,hajajipanga nampa Onyo kupitia RUWASA Mkoa pamoja na RUWASA Makao makuu wamsimamie huyu ili aweze kutekelza makubaliano ya mkataba na sio kuleta visingizio”alisema RC Mrindoko.
Mhe.Mrindoko amebanisha kuwa changamoto nyingine ni RUWASA Makao makuu wenyewe ambao wamekuwa chanzo cha kusuasua mradi huo kutokana na kuchelewa kujibu Burua ambazo mara kadhaa wamekuwa wakiandikiwa na RUWASA Ngazi ya Mkoa.
“Nimesikia hapa barua zinaandikwa mawasiliano yanafanyika na RUWASA Makao makuu lakini hawajibu chochote. Niombe RUWASA Makao makuu niombe Wizara ya Maji, Vijiji 16 vina changamoto ya Maji hapa Mlele kwa sababu mradi huu haukamiliki kwa wakati hatuwezi kuendelea namna hii.”alisema RC Mrindoko.
Kutoka na changamoto hiyo Mhe.Mrindoko ametoa Ombi kwa RUWASA Makao Makuu pamoja na Wizara ya Maji kufika katika Mradi huo kutatua changamoto zilizopo ili Wananchi waondokane na changamoto ya upatikanaji wa Maji katika Wilaya ya Mlele.
Aidha Mhe.Mrindoko pia ametoa maelekezo kwa RUWASA Mkoa wa Katavi kumsimamia kwa karibu Mkandarasi HEMATEC Investment LTD anayeteleleza mradi huo ili aweze kutekeleza mradi huo kwa viwango na ubora unaotakiwa.
Kwa Upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mlele Bw.Gilbert Isack ameeleza kuwa mradi huo ambao utazalisha Lita Bilioni 2 za Maji kwa mwaka kwa sasa uko katika hatua za Mwisho za ukamilishaji ambapo pindi mradi huo wenye thamani ya Shilingi Bilioni 2.8 utakapokamilika utaondoa adha ya Maji kwa wakazi takribani 68,000 kwa Vijiji 16 Wilayani Mlele.
MATUKIO KATIKA PICHA
Picha 1:Muonekano wa Bwawa la Nsenkwa lililoko Kijiji cha Nsenkwa Kata ya Nsenkwa Halmashauri ya Wilaya ya Mlele linalotegemewa na Wakazi wa Wilaya ya Mlele kama chanzo kikuu cha Maji.
Picha 2:Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Philberto Sanga akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko alipotembelea Mradi wa Maji wa Bwawa la Nsenkwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mlele 27 Agosti 2022.
Picha 3:Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa akiomba ufafanuzi kutoka kwa Mwakilishi wa Mkandarasi Kampuni ya HEMATEC Investment LTD inayoteleleza Ujenzi wa Mradi wa Bwala la Nsenkwa katika Ziara ya RC Katavi kukagua Miradi 27 Agosti 2022.
Picha4:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrondoko akipokea maelezo kuhusu Mradi kutoka kwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Mlele alipotembelea mradi wa Maji wa Ujenzi wa Bwawa la Nsenkwa 27 Agosti 2022
Picha 5:Mwakilishi wa Kampuni ya HEMATEC Investment inayotelekeza Mradi wa Ujenzi wa Bwawa la Nsenkwa akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko katika ziara hiyo 27 Agosti 2022
Picha 6:Meneja wa RUWASA Mkoa wa Katavi akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko kuhusu utekelezaji wa Mradi wa Maji wa Bwawa la Nsenkwa.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved