Kiongozi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko amekabidhi mitambo ya magari 2 ya kuchimba visima vya maji kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) kwa ajili ya mkoa wake.
Mhe. Mrindoko amesema mitambo ya magari hayo imetokana na programu ya UVIKO 19 iliyotenga fedha pamoja na mambo mengine kwa ajili ya ununuzi wa mitambo ya uchimbaji wa visima vya maji.
Amesema ujio wa mitambo hiyo utarahisisha na kuongeza juhudi za utoaji wa huduma ya maji vijijini kwa sababu mkoa utakapokuwa na uhitaji wa uchimbaji wa visima vya maji hakutakuwa na shida ya upatikanaji wa vifaa, vifaa vitakuwepo.
Mhe. Mrindoko amesema seti ya mitambo hiyo, iliyo na uwezo kuchimba visima hadi mita 400 kwenda chini ya ardhi, imeshachimba tayari visima 12 katika Mkoa wake ajili ya wananchi wa mkoa huo.
Mbele ya mwakilishi wa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Katavi, aliyehudhuria katika hafla ya makabidhiano ya magari hayo, Mhe. Mrindoko amemuhakikishia kiongozi huyo kuwa, ufikiaji wa lengo la utoaji wa maji wa 85% ifikapo 2025 kwa wananchi wa vijijini, utafikiwa bila chenga kwa sababu mkoa umejipanga vizuri.
Upatikanaji wa maji kwa sasa katika Mkoa wa Katavi ni 70.9 na juhudi zinaendelea kuhakikisha kuwa huduma hii inamfikia mwananchi hapo alipo.
Kisha kukabidhi mitambo hiyo, Mhe Mrindoko ameielekeza RUWASA kuitumia mitambo hiyo kwa ajili ya kuchimba visima, kukarabati na kufufua visima kwa ajili ya wananchi wake na si kwa malengo mengine.
Amewataka pia wananchi kutunza vyanzo maji na miradi ya maji iliopo ili iweze kuendelea kutoa huduma iliyokusudiwa
Maji ni kitu cha msingi sana katika maisha ya viumbe na maendeleo duniani, hatuna budi kuvitunza vyanzo vya maji na mzingira yetu ili rasilimali hii iweze kutusaidia sisi wanadamu.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved