ADUI MARADHI ABANWA MBAVU MKOANI KATAVI
Afya bora ni nguzo na rasilimali muhimu katika kuchangia maendeleo ya mtu binafsi, familia na nchi hususani katika kuleta maisha bora na kupunguza umaskini. Maenendeleo ya nchi yetu yataletwa na wananchi wenye afya na uwezo wa kuzalisha mali
Afya bora ni haki ya msingi ya binadamu na kiungo muhimu cha kufanikisha ajenda ya maendeleo enedelevu ifikapo 2030
Serikali yoyote duniani ina jukumu la kuandaa watalaam wa mambo ya afya, kujenga hospitali na miundombinu mingine ya afya kwa ajili ya wananchi wake. Aidha ina jukumu la kutoa dawa na vifaa tiba
Zaidi ya miongo 5 tukiwa ndani ya muungano wa Tanzania, sisi kama nchi tumeendeleza mapambano dhidi ya adui maradhi kwa kujenga miundombinu ya afya, kutoa madawa na vifaa tiba kwa ajili ya ustawi wa afya ya mwananchi wetu
Leo Kiongozi Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko amezindua Jengo la Mionzi na Wodi ya Watoto na wanawake katika kituo cha Afya Ilembo ili kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya maradhi katika mkoa wake.
Ujenzi wa Jengo la Wodi ya watoto, wanawake na wanaume, Jengo la Mionzi na X-Ray vimegharimu mil. 457.
Hadi sasa serikali mkoani Katavi ina Hospitali 1 ya Rufaa, Hospitali 5 za Halmashauri, vituo vya vya afya 23 na zahanati 94. Hivyo jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya ni 123. Hospitali, vituo vya afya pamoja na zahanati vyote vinatoa huduma kwa wananchi.
Kwa upande wa madawa na vifaa tiba vinapatikana huku serikali ikiongeza juhudi za kuongeza watumishi wa afya kila mwaka ili kuboresha zaidi huduma ya afya katika mkoa
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved