Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amewataka wanawake na jamii kutumia maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kusambaza maadili na tabia njema katika mkoa wake na taifa kwa ujumla.
Mhe. Mrindoko amesema hayo leo katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Mpanda Ndogo katika Wilaya ya Tanganyika.
Amesema tumeshuhudia mmomonyoko wa maadili katika jamii yetu; kuna ajira za watoto wadogo, mimba za utotoni na vitendo mbali mbali vya ukatili kama vile ubakaji, ulawiti katika jamii yetu.
Kufuatia changamoto hizo, kiongozi huyo amewataka wazazi na walezi kujitathmini kuona mahali ambapo wamekosea na kuchukua hatua za makusudi kujirudi na kupaza sauti zao kwa pamoja kukemea na kupiga vita vitendo vyote vya ukatili katika jamii yetu.
Mhe. Mrindoko ameelezea kuwa wanawake wana mchango mkubwa sana katika jamii; wanapaswa pamoja na mambo mengine kulea watoto katika maadili mema, kusambaza upendo, utulivu na amani katika familia na jamii ili kujenga taifa adilifu na raia wema.
Amewataka wanawake kuitumia vizuri nafasi kubwa waliyonayo katika jamii kujenga na kuimarisha utu wema katika familia zao na baadae kuyapeleka malezo hayo kwa jamii.
Wakati huo huo, Mhe Mrindoko amewataka wanwake, walemavu na vijana kuchangamkia na kutumia fursa mbali mbali zinazopatika katika Mkoa wa Katavi kwa ajili kujiendeleza kiuchumi na kijamii.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved