Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari Mkoani Katavi wametakiwa kutumia fursa ya maboresho ya miundombinu ya Elimu Mkoani humo kujituma katika masomo yao ili kuinua ubora wa Elimu na hivyo kutimiza azma ya Serikali ya awamu ya sita ya kuinua ubora Nchini.
Akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lyamba 9 Septemba 2022 mara baada ya kukagua Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa yanayojengwa Shuleni hapo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Mrindoko amewaambia Wanafunzi hao kuwa Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan inaboresha miundombinu ya Elimu ili kuwajengea mazingira wezeshi ya kufanya vizuri zaidi katika masomo yao hivyo ni wajibu wao kutumia fursa hiyo kujituma ili kufanya vizuri zaidi katika masomo yao.
Amewaambia Wanafunzi hao kuwa lengo la Serikali ya awamu ya Sita ni kuhakikisha kuwa watoto wote wanaohitimu darasa la saba wanapata fursa ya kupata Elimu ya Sekondari ili iweze kuwasaidia kujikwamua katika maisha yao.
Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari Lyamba,Mkuu wa Shule hiyo Bi.Aanastasia Muna amesema Shule hiyo ilipokea Kiasi cha Shilingi Milioni 100 kwa ajili ya kutekeleza Ujenzi wa Vyumba 5 vya Madarasa ambapo mpaka sasa utekelzaji wa ujenzi huo uko asilimia 40.
Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza Qeen Mwalukasa akizungumza kwa niaba ya Wanafunzi Shuleni hapo amemshukuru Mhe.Rais Samia Suhuhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya Madarasa Shuleni hapo ambapo ameahidi kujituma zaidi katika masomo yao.
Shule ya Sekondari Lyamba ni moja kati ya Shule 14 za Sekondari za Serikali ndani ya Manispaa ya Mpanda.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved