• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

RC Katavi ardihishwa na Ujenzi wa Madarasa ya Rais Samia Manispaa ya Mpanda, Awataka watumishi wa Umma kuwa waadilifu,kukamilisha Miradi kwa wakati.

Posted on: November 10th, 2022

Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akikagua ujenzi wa Madarasa katika Shule ya Sekondari Lyamba iliyoko Manispaa ya Mpanda 09 Novemba 2022


Mpanda.

Watumishi wa Umma Mkoani Katavi wametakiwa kuwa waadilifu wakati wa usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuhakikisha kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo inakamilika kwa ubora na viwango vinavyotakiwa.

Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko  10 Novemba 2022 wakati akikagua Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa maarufu kama Madarasa ya Rais Samia katika Manispaa ya Mpanda ikiwa ni utekelezaji wa ratiba ya kamati ya ulinzi na Usalama Mkoani humo  kufuatilia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Kwa Sasa hivi tunafuatilia ujenzi huu wa madarasa ya Rais Samia ili kuhakikisha kuwa Ujenzi wa Madarasa yanakamilika ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unaotakiwa.Maelekezo ya Mhe.Rais ni kukamilisha madarasa haya Tarehe 15 Desemba 2022 lakini sisi Mkoa wa Katavi tunasema tutakamilisha Ujenzi huu Tarehe 07 Desemba 2022 ili ile wiki moja iwe ni ya Waziri wa TAMISEMI kufanya ufuatiliaji  na kumkabidhi Mhe.Rais.”Alisema Mkuu wa Mkoa Mrindoko.

 Bi.Mrindoko  ameipongeza Manispaa ya Mpanda kwa kusimamia vizuri Ujenzi wa madarasa ya Mhe.Rais Samia ambapo amewataka kuongeza jitihada zaidi ili kuhakikisha kuwa Ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliopangwa.

“Nyie Manispaa ya Mpanda mnaongoza kwa kuwa na vyumba vingi vya madarasa na mna vyumba 51 kati ya 119 na katika maeneo niliyopitia nimeridhishwa na hatua nzuri ya ujenzi hivyo msibweteke na sifa na badala yake mjipange kuhakikisha kuwa mnakamilisha Ujenzi ndani ya muda uliopangwa”alisema Bi.Mrindoko.

Aidha Bi Mrindoko ametoa rai kwa Wananchi kuendelea kuchangia nguvu kazi katika Ujenzi wa Madarasa 119 ili Shilingi Milioni Ishirini iliyotolewa kwa kila darasa itosheleze kumaliza ujenzi huo ambapo amewataka Wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa kia darasa ndani kunakuwepo na viti na meza kwa ajili ya Wanafunzi.

 Nae Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bi Jamila Yusuf Kimaro amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa Katavi kufanya ufuatiliaji wa karibu muda wote ili kuhakikisha kuwa Ujenzi huo unakamilika ndani ya muda uliojiwekea Mkoa.

Akiwa Manipaa ya Mpanda Mkuu wa Mkoa Bi Mwanamvua Mrindoko amekagua Ujenzi wa Vyumba vya madarasa katika Shule za Sekondari Lyamba,Rungwa,Shanwe,pamoja na Mpanda Day.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO AZINDUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2025

    May 05, 2025
  • RC MRINDOKO AIHAKIKISHIA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MKOANI KATAVI.

    April 29, 2025
  • WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA MIKAKATI YA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA WESTERN, KITONGOJI CHA LUHAFWE – H/ WILAYA YA TANGANYIKA

    April 24, 2025
  • PPPC WATOA ELIMU UIBUAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA UBIA.

    April 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved