Pichani: Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akimkabidhi zawadi ya Cheti Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe.Filberto Sanga baada ya Wilaya ya Mlele kutangazwa kufanya vizuri katika suala la Utunzani wa Mazingira.
Mpanda- Katavi.
Ili kudhibiti uharibifu wa mazingira na kuzuia magonjwa ya mlipuko, Mkuu wa mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko amekemea vikali tabia ya baadhi ya Wananchi kuosha vyombo vyao vya Moto ndani ya mito na badala yake amewataka kutafuta maeneo mengine na kuweka miundombinu ya Maji ili kufanya kazi yao hiyo
RC Mrindoko amepiga marufuku hiyo 10 Oktoba katika kikao cha tathimini ya utekelezaji wa mpango mkakati wa usafi na utunzaji mazingira mkoa wa Katavi,kilichowakutanisha Viongozi mbalimbali wakiwemo wa Dini, Serikali sambamba na wadau mbalimbali.
"Nimarufuku na suala hili lisimamiwe na likomeshwe kabisa. Tuache vyanzo vya maji vitumike kwa matumizi mazuri....hata kama utakuta gari langu pale limeandikwa RC Katavi,ukimkuta (Dereva) anaosha kule kamata hilo gari"
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Mkuu wa Mkoa,wadau wamependekeza na kupitisha kila kaya kupatiwa miche 5 ya miti Kwa ajili ya kupanda ili kuendelea kutunza mazingira sanajri na kila Taasisi kupewa miche kuanzia 20,hiyo ikiongezeka kutokana na ukubwa wa Taasisi husika kama TANROAD,TARURA,RUWASA n.k
Kupitia mkakati uliozinduliwa Mwezi April wa "Ngarisha Katavi,tunza mazingira" katika kipengele cha mazingira kikizitaka kila Halmashauri kupanda miche Milioni 1.5 kwa kila mwaka,RC Mrindoko ameziagiza Halmashauri zote kutekeleza agizo hilo kwa kuanzisha vitalu visivyopungua miche hiyo kwa kuwa ni takwa la kisheria na sera ya mazingira.
Katika hatua nyingine,RC Mrindoko amesainiana na kukabidhi mikataba ya Lishe na wakuu wa Wilaya za mkoa huo lengo likiwa ni utekelezaji wa kupambana na lishe duni kuanzia ngazi ya Wilaya hadi ngazi ya kitongoji.
Kutokana na tathimini ya Sita ya Mwaka 2021 ya Lishe, Mkoa wa Katavi uko nafasi ya 14 Kitaifa huku sababu ya nfasi hiyo ikitajwa kuwa ni pamoja na Halmashauri za Mkoa huo kushindwa kutoa fedha za afua za Lishe kama ilivyoainishwa kwenye Bajeti na mipango.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved