• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua pepe za Watumishi |
Katavi Regional Website
Katavi Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Katavi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Maono na Dhamira
  • Huduma
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na bRasilimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Halmashauri
      • Miundombinu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • maji
      • Afya
      • Elimu
    • Vitengo
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Idara ya Fedha na Uhasibu
      • Manunuzi
      • Sheria
      • Mkaguzi wa Ndani
    • Muundo wa Taasisi
  • Machapisho
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Videos
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Wilaya
    • Mpanda
    • Mlele
    • Tanganyika
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Livestock
    • Industry and Fishing
    • Minerals
    • Fishing
  • Utalii
    • Katavi National Park
    • Nkondwe Waterfalls
  • Biashara

RC Katavi aonya upotoshaji sensa ya watu na makazi.

Posted on: August 15th, 2022

Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko(katikati)  ,Katibu tawala Mkoa wa Katavi Bw.Abas Rugwa(kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mpanda(kulia)waliposhiriki matembezi katika bonanza lililoandaliwa kwa ajili ya kuhamasisha Wananchi kushiriki katika Sensa ya watu na makazi 23 Agosti 2022.

Mpanda -Katavi  

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameitaka jamii kuepukana na upotoshaji unaofanywa na baadhi ya watu kuhusu sensa ya watu na makazi.

Akizungumza na hadhara ya wananchi  Agosti 15, 2022 katika bonanza la kuhamasisha wananchi kushiriki sensa, Mwanamvua amesema wakibaini watu wenye tabia hiyo watoe taarifa kwa viongozi na vyombo vya dola wachukuliwe hatua.

"Tutashughulika nao vizuri kisheria hatutawaacha salama kwasababu watakuwa hawana nia nzuri na rais," amesema.

Aidha amewataka wananchi kutowaficha watu wenye ulemavu, wanatakiwa kuhesabiwa ili watengenezewe utaratibu mzuri wa kupata huduma.

"Kupitia bonanza hili tulilofanya natumia nafasi hii kutangaza kuwa sasa tunao mabalozi wa sensa kupitia makundi yetu maalumu.

"Tunao bodaboda, bajaji, wajasiriamali, machinga na wengine tunawakabidhi kazi hii ya kuhamasisha sensa mkaifanye kupitia mabango na kuzungumza na wateja wenu," amesema,

Naye Ally Hamis ambaye ni mkazi wa Manispaa ya Mpanda amesema bonanza hilo limeongeza uelewa kuhusu masuala ya sensa kutokana na elimu iliyotolewa.

"Tunaenda kuhamasisha wengine wahesabiwe ili serikali ipate idadi kamili rai yangu watu wajitokeze tarehe 23, tukihesabiwa ni faida yetu sisi," amesema.

Bonanza hilo lilofanyika viwanja vya Azimio Manispaa ya Mpanda limeambatana na matembezi ya hiari, michezo ya mpira wa miguu na kuvuta kamba lengo ni kuhamasisha jamii kushiriki sensa.



Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI DESEMBA 2024 December 12, 2024
  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA 2025 December 16, 2024
  • MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2024 January 04, 2025
  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 January 04, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RC MRINDOKO AZINDUA MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2025

    May 05, 2025
  • RC MRINDOKO AIHAKIKISHIA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI USALAMA WA UCHAGUZI MKOANI KATAVI.

    April 29, 2025
  • WAZIRI NDEJEMBI AONGOZA MIKAKATI YA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI ENEO LA WESTERN, KITONGOJI CHA LUHAFWE – H/ WILAYA YA TANGANYIKA

    April 24, 2025
  • PPPC WATOA ELIMU UIBUAJI WA MIRADI INAYOTEKELEZWA KWA UBIA.

    April 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

UZINDUZI RATIBA YA SAFARI ZA NDEGE ATCL SIKU YA JUMATATU 23 MEI 2022
Video zinginezo

Wavuti wa Haraka

  • SALARY SLIP PORTAL
  • FURSA ZA UTALII KATUMA MKOANI KATAVI
  • KATAVI RS HABARI
  • KATAVI RS HABARI YOUTUBE

Wavuti mwambata

  • Mpanda Municipal Council
  • Mpimbwe District Council
  • Mpanda District Council
  • Nsimbo District Council
  • Mlele District Council
  • Tovuti ya utumishi

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

click here

Ramani

Wasiliana nasi

    Mpanda-Katavi (Mkoani Area)

    Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi

    simu: 025-2957108

    Mobile:

    Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera za Falagha
    • Kanusho
    • Maswali ya mara kwa mara
    • ramani
    • Huduma

Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved