Na:OMM Katavi.
Serikali Mkoani Katavi imeendelea na utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan la kupanda miti ambapo takribani miti Milioni 4.7 imepandwa katika meneo mbalimbali kupitia kampeni Maalumu ya Ng'arisha Katavi tunza mazingira iliyoanza Tarehe 24/1/2023.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko 26 Januari aliwaongoza Viongozi na Wananchi Mkoani humo kupanda Miti katika Bwawa la Mto Milala Manispaa ya Mpanda ikiwa ni uzinduzi rasmi wa Kampeni endelevu ya Upandaji wa Miti almaarufu “Ng'arisha katavi tunza Mazingira” iliyoanza kutekelezwa katika ngazi ya Wilaya Tangu 24 Januari 2023.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Kampeni hiyo ya Upandaji mti Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema Hadi sasa takribani miti 4.7 imepandwa katika maeneo mbalimbali Mkoani humo ambapo lengo ni kufikia lengo la Upandaji wa Miti Milioni 10 kwa Mwaka 2023.
“Kwa mwaka 2023 lengo letu ni kupanda miti Milioni 10 mpaka sasa tumepanda miti zaidi ya milioni 4.7 kwenye halmsahauri zote kwenye taasisi za shule msingi na sekondari pamoja na kaya za mtu mmoja mmoja'' amesema Mrindoko.
Mkuu wa Mkoa Mrindoko amewahimiza Wananchi Mkoani Katavi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao ya makazi ikiwa nisehemu ya kuunga mkono juhudi za serikali katika utunzaji wa Mazingira.
Mrindoko akiwa katika Bwawa la Milala amepiga marufuku kufanya Kazi yeyote ya kibinadamu kwenye chanzo hicho kwa kuwa ndicho chanzo kikuu Cha maji katika Mradi wa maji wa miji 28 ambao mkoa wa katavi nisehemu ya wanufaika na Mradi huo pindi utakapoanza kutekelezwa.
“Nitumie nafasi hii kupiga marufuku na kukataza kabisa shuguli za kibinadamu kuzunguka Bwawa la Milala kulima,Kuchunga Ngo”mbe,Kufuga,Kuvua Samaki,na kufanya shuguli nyingine ni marufuku nimesema bwawa hili ni bwawa mhimu nichanzo cha maji na ttutakilinda na kukitunza kwa kushirikiana na wanachi waliopo maeneo haya”
Katika hatua nyingine amewaomba wananchi walio karibu na Chanzo hicho Bwawa la Milala kuwa Mabalozi na walinzi wa vyanzo hivyo Kwa kutoa taarifa za Kwa mamlaka husika kama Kuna kiashria Cha uharibu wa mazingira na vyanzo vya maji kwenye bwawa Hilo zinazofanywa na binadamu.
Awali akitoa taarifa Kwa Mkuu wa mkoa wa Katavi Kaimu Mkurugenzi wa Muwasa Manispaa ya Mpanda Justini Wambali amesema katika kulinda chanzo hicho Cha maji wamekuwa wakishirikiana Kwa pamoja na wananchi kukilinda chanzo hicho kwa kutokufanya shughuli za kibinadamu.
Wambali ameeleza kuwa katika Mradi wa maji wa miji 28 utakwenda kuwa mkombozi wa utoaji wa huduma ya maji kwa wanachi wa Manispaa ya Mpanda kwani tayari mikataba baina ya serikali na wafadhili kutoka Serikali ya India ulishasainiwa tayari kwa utekelezaji kwa Gharama ya shilingi Bilioni 22.
"Mradi wa ujenzi wa Bwawa la Milala unakwenda kutatua kero ya upatikanaji ya huduma ya maji kwa wananchi wa Manispaa ya Mpanda kwa asilimia mia moja kwa kuongeza uzalishaji wa maji kutoka Lita Milioni 6 na elfu 50 kwa siku hadi kufikia lita Milioni 19 na elfu 50 kwa siku ambapo mahitaji ya maji kwa kata 15 za Manispaa ya Mpanda ni lita Milioni 15".
Amesema Kwa Sasa bwawa Hilo linatumika kama chanzo cha Maji Kwa kutoa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo ya kata ya shanwe na Eneo la chuo Cha Veta Mpanda.
Hamisi Mrisho mkazi wa Bwawani amesema aungamkono agizo la mkuu wa Mkoa la kupiga marufuku kazi za kibinadamu kwenye Bwawa la Milala na kuhakikisha wao kama wakazi wa eneo jirani na chanzo hicho cha bwawa watakuwa sehemu ya kulinda na Kutunza vyanzo vya Maji kwa vitendo.
‘’Kwa kuwa zoezi hili la upandaji miti ni endelevu naunga mkono agizo la Mkuu wa mkoa” amesema Mrisho.
Kwa upande wake Anjelina Lucas mkazi wa kivukoni akiwa katika chanzo hicho Cha maji Cha bwawa la Milala amesema Kila mwanananchi anawajibu wa kutunza Mazingira Ili kulinda vyanzo vya maji.
"Tumeshiriki kupanda miti kwenye Bwawa hili na sisi kama wananchi tupo Pamoja na Serikali kutunza rasilimali maji Kwa kutunza Mazingira na kupanda miti’’ .
Kampeni ya kupanda miti katika mkoa wa katavi inayojulikana kama Ng'alisha katavi tunza Mazingira inalengo mahususi ya kulinda mazingira na vyanzo vya maji kama sehemu ya tekelezo agizo la Serikali la kupanda miti kama sehemu ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved