Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko leo Novemba 26, 2024 ametembelea na kukagua ujenzi wa jengo la kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Katavi.
Akizungumza baada ya kukagua mradi huo Mhe. Mrindoko amepongeza maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho huku akisisitiza matumizi ya fedha kutumika ipasavyo kwa malengo ya ukamilishaji wa jengo kama ilivyoelekezwa katika mchanganuo.
Awali akitoa tarifa ya ujenzi wa jengo hilo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Lilian Wana amesema ujenzi huo ulianza Desemba 01, 2023 na umefikia asilimia 46% huku changamoto kubwa ikiwa ni ucheleweshwaji wa fedha kutoka hazina kuu na mabadiliko ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved