Pichani:Katbu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa akizungumza na Wananchi wa Kata ya Mwamapuli katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko 27 Agosti 2022.
Mpimbwe –Katavi
Wakulima wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Wilayani Mlele wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujisajili ili waweze kunufaika na mbolea ya Ruzuku.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Hassan Abas Rugwa 27 Agosti 2022 katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko kukagua miradi ya maendeleo katika eneo la Mwamapuli.
Bw.Rugwa amewaambia Wananchi wa Kata ya Mwamapuli kuwa wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi likiendelea Nchini liko pia zoezi la usajili wa Wakulima kwa ajili ya kupata mbolea ya Ruzuku ambapo amewataka kutoa ushirikiano kwa kujisajili kwa kuwa mbolea hiyo itatolewa kwa Wakulima waliojisajili peke yake.
Ameeleza kuwa lengo la Serikali kulipia karibia nusu ya bei ya pembejeo hizo za kilimo ni kujenga mazingira wezeshi kwa wakulima ili kuleta tija katika uzalishaji na hivyo kuwakwamua Wananchi hususani wakulima na Umasikini.
“Mhe.Rais amelipia karibia nusu ya bei ya mbolea na hiyo pesa ambayo Mhe.Rais ameilipia hautadaiwa wala kukatwa kinachotakiwa ni wewe kujisajili ili kuweza kunufaika na pembejeo hizo”alisema katibu tawala Rugwa.
Mnamo Tarehe 17 Mei 2022 Waziri wa Kilimo Bw.Hussein Bashe katika hotuba yake Bungeni katika kikao cha 13 Mjini Dodoma alieleza kuwa Shilingi Bilioni 150 zimetengwa na Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa ajili ya kutoa Ruzuku ya mbolea kwa wakulima wa mazao yote Nchini kwa masimu wa Kilimo 2022/2023.
Tayari katika baadhi ya maeneo Nchini Wakulima wamejisajili na wameanza kupata Mbolea ya Ruzuku.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved