MKUU WA MKOA MSTAAFU MUHUGA AFANIKIWA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS LA MABASI KUSAFIRI BILA ESKOTI YA POLISI
Na Walter Mguluchuma - Katavi .
Mkuu wa Mkoa mstaafu wa Mkoa wa Katavi Meja Generali Mstaafu Raphael Muhuga ameseme kuwa katika kipindi chake cha uongozi katika Mkoa huo amefanikiwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli alilomtaka kuhakikisha mabasi yote yanayoingia na kutoka nje ya Mkoa huo yanafanya safari zake bila kuwa na eskoti ya Polisi.
Mbali ya mabasi kufanya safari zake bila eskoti pia ameweza kufanikiwa kuimarisha ulinzi katika maeneo yote ya Mkoa huo yanayopakana na Nchi za Kongo na Burundi hari ambayo imefanya waweze kuzuia biashara zote haramu zilizokuwa zikifanyika katika maeneo ya mipakani hapo awali .
Muhuga amesema hayo hapo wakati wa ibada ya misa ya pili iliyofanyika katika kanisa kuu la Mtakatifu Maria Imakulata Jimbo Katoliki la Mpanda wakati akiwahutubia waumini wa kanisa hilo alipokuwa akiwaaga katika ibada iliyoongozwa na Katibu wa Jimbo hilo Padri Anakretus Bafumkeko .
Amesema wakati Rais alipomteuwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi mwaka 2016 alimwagiza ahakikishe anamaliza kabisa tatizo la utekwaji wa magari ya abiria uliokuwa ukifanyika katika Mkoa huu na kusababisha mabasi yote yalikuwa yakitoka na kuingia
kwenye Mkoa huu kuwa nanaposafiri kuwa na eskoti ya polisi wenye silaha za moto .
Alifafanua kuwa katika kipindi chake cha uongozi uliodumu kwa kipindi cha miaka miwili na miezi minne hadi kustaafu kwake mwezi huu ameweza kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwenye vyombo vya ulinzi na usalama vya Mkoa hari ambayo imeweza kufanya aweze kutekeleza agizo hilo alilopewa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli .
Mbali na kufanikiwa kuimarisha ulinzi vyombo hivyo pia vimesaidia kuondoa tatizo lilikuwapo awali la biashara haramu zilizokuwa zikifanywa kwenye maeneo ya mipakani .
Muhuga amesema Mkoa wa Katavi unakabiliwa na baadhi ya changamoto mbalimbali ambazo amehahidi kumwachia kwa maandishi Mkuu wa Mkoa mpya Amos Makala atakapo kuwa anamkabidhi ofisi ili nae aweze kuangalia namna ya kuendelea kuzitatua .
Alieleza kuwa miongoni mwa changamoto zilizopo katika Mkoa huo ni tatizo la mimba za utotoni ambapo Mkoa huo ndio unao ongoza kwa kuwa na mimba za utotoni ambapo Mkoa una asilimia 45 ya wasichana kupata mimba za utotoni .
Changamoto nyingine aliitaja kuwa Mkoa huo kuwa na idadi kubwa ya wanawake wasio jua kusoma na kuandika ambapo wanawake wastani wa asilimia 33 hawajuwi kusoma na kuandika .
Vilevile tatizo la uharibifu wa mazingira unaofanywa na wafugaji wanaoingia kwa wingi kutoka Mikoa ya Kanda ya ziwa ambao wamekuwa wakikata misitu ovyo na kufugia mifugo kwenye maeneo yasiyo sitahili .
Nae Katibu wa Jimbo Padri Pafumkeko aliwataka wakazi wa Mkoa wa Katavi kumuenzi Mkuu huyo wa Mkoa kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kuimarisha ulinzi katika Mkoa wa Katavi na katika jitihada zake za kuleta maendeleo katika Mkoa huo .
Alisema Muhuga alifanya kazi zake kwa uadilifu mkubwa na ndio maana ameweze kustaafu akiwa mtumishi aliyetukuka kwani ameweza kustaafu mara mbili yaani jeshini na kwenye nafasi ya ukuu wa Mkoa .
Aliwataka wananchi wa mkoa huo kutoa ushirikiano kwa mkuu wa Mkoa mpya kama ambavyo walivyotoa ushirikiano kwa mkuu wa Mkoa aliyestaafu .
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved