Pichani:Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko akikabidhi Trekta kwa Mkulima kutoka Wilaya ya Mlele lililotolewa kama Mkopo kwa Mkulima huyo kutoka Benki ya NMB wakati wa uzinduzi wa Msimu wa Kilimo katika kilele cha Wiki ya Mwanakatavi 2 Novemba 2022.
Mpanda.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko ametoa rai kwa Wananchi Mkoani humo kutunza chakula cha kutosha kutokana na tishio la uwepo wa mvua chini ya Wastani katika msimu wa wa Kilimo 2022/2023.
Mhe.Mrindoko ametoa rai hiyo katika tukio la uzinduzi wa Msimu wa Kilimo ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii iliyohitimishwa rasmi 2 Novemba 2022 katika uwanja wa Shule ya Msingi Kashato Manispaa ya Mpanda.
“Katika maeneo mengine ikiwemo Nchi jirani hali si shwari kun njaa ya hali ya juu,Niwaombe sana Wananchi wa Mkoa wa Katavi kila kaya ihakikishe inatunza chakula cha kutosha ikiwa ni tahadhari ya hali ya ukame”alisema Bi Mrindoko.
Mkuu wa Mkoa Mrindoko ameeleza kuwa Mkoa wa Katavi katika msimu mpya wa Kilimo 2022/2023 umedhamiria kulima Ekari 339,187 zikiwemo hekta 273,436 za mazao ya chakula na Hekta 65752 za Mazao ya Biashara.
Ameeleza kuwa lengo la Mkoa kwa Msimu wa Kilimo 2022/2023 ni kuzalisha tani 1,159,754 ikiwemo tani 1,074,187 za mazao ya chakula na tani 85,568 za mazao ya Biashara ambapo mahitaji ya mbolea ni tani 14,811.
Katika hatua nyingine Bi Mrindoko amewataka Wananchi Mkoani Katavi kujitokeza kwa wingi kujisajili katika Daftari la Wakulima ili waweze kunufaika na Mbolea ya Ruzuku ili kuleta tija katika uzalishaji.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved