MRADI WA MIOMBOMBO MKOMBOZI KWA WANANCHI
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jenerali (Mst) Raphael Muhuga amewataka Vijana wa Mkoa wa Katavi kutumia fursa waliyoipata ya kuwa na mashine ya kusindika mafuta ya alizeti na mashine ya kuchakata asali, iwapo watatumia fursa hiyo itaweza kuwainua kiuchumi kwa kuwaongezea kipato na kukuza uchumi kwa ujumla wa mtu mmoja moja Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Meja Muhuga ametoa rai hiyo muda mfupi baada ya kuweka jiwe la msingi kwenye jengo la kikundi cha vijana kinachojihusisha na usindikaji mafuta ya alizeti Kalovya - Inyonga Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kikundi kinachofadhiliwa na Shirika la maendeleo ya umoja wa Mataifa kupitia mradi wa kuhifadhi misitu ya miombo.
Amesema kikundi kitanufaika iwapo wataweza kukitumia kwa makusudi yaliyokusudiwa kwa kuwa wamepata mradi endelevu, na wakulima wote wa mkoa wa katavi watatumia fursa hiyo kujikomboa na kuwasihi watumie vizuri na waitunze ili iweze kuwanufaisha na kuwaletea faida.
Naye Robart Berege Mwenyekiti wa kikundi anaeleza mafanikio waliyoyapata kutokana na uwepo wa mashine hiyo na wao kama kikundi, awali walipata changamoto kwa kuwa walikuwa hawajui hatima yao ya baadae lakini baada ya mradi wa miombo kuwapatia elimu na kuwasaidia kupata elimu wamesema imewasaidia sana na kutoa wito kwa jamii kuachana na kilimo cha tumbaku badala yake wajikite katika kilimo cha alizeti kwa kuwa ni kilimo cha zao rafiki na wala hakiharibu mazingira na ndiyo lengo la mradi wa miombo kuhifadhi mazingira.
Mapema Mratibu wa Kanda ya Magharibi wa mradi wa miombo Yobu Kiungo katika taarifa yake alieleza kuwa kikundi kina jumla ya wanakikundi tisa kati yao wanaume sita na wanawake watatu, katika kukamilisha mradi kikundi kilichangia ujenzi wa jengo kwa gharama ya shilingi milioni nane na mradi wa miombo uliwezesha jumla ya shilingi milioni 28,365,213.
Amesema kisia cha shilingi milioni tisa na elfu hamisini na mbili mia saba hamsini na tatu zimetumika kuweka umeme kupaka rangi na sakafu, kupiga lipu na kujenga vyoo na kuweka uzio kuzunguka jengo pamoja na kuweka matenki kwa ajili ya kuhifadhi mazingira wakati wa kipindi cha mvua mradi wa maji na kuwa na tanki la kuhifadhia maji. jumla ya thamani ya mradi huu ikiwemo mchango wa kikundi ni shilingi milioni 36, 365 213.
Pia mradi wa miombo umekiwezasha kikundi hiki magereni 1000 ya lita tano kama mtaji wa kuanzia kuweka mafuta, ndoo 150 za lita 20 pia kwa kuanzia imeonekena wawe na nembo yao mradi kwa kushirikia na Wilaya wameweza kubuni nembo ambao wamepatiwa lebo 650, kati ya hizo 500 zitakuwa kwenye lita tano na 150 zitakuwa kwenye lita 20.
Akizungumzia uwezo wa mashine ameeleza kuwa ina uwezo wa kukamua kiasi cha tani 2.5 hadi tatu sawa na maguni hamsini hadi sitini kwa siku kwa muda wa masaa nane, mradi huu unatarajio la kuondoa changamoto ya ukosefu wa soko la zao la alizeti kwa kuwa watakuwa wanauza mafuta na jumla ya vijiji vilivyopo katika mradi ni tisa lakini vijiji vyote vilivyopo katika Wilaya ya Mlele vitakuwa vinatumia mashine hii, pia imefanyiwa majaribio na inauwezo hata wa kuchunja mafuta ya karanga na maboga.
Kuhusu mashine ya uchakataji asali mratibu huyo ameleza kuwa, Mradi umewezeshwa fedha na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP imenunua mashine ya kuchakata asali kiasi cha shilingi milioni 170, ambazo zimetumika kwa ajili ya ununuzi wa mashine kuisimika pamoja na mafunzo.
Pia ameeleza kuwa iwapo mashine itasimamiwa na kuonesha matokeo mazuri fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya usimamizi milioni 60 za uendeshaji zinaweza kutolewa, iwapo Wilaya na Mkoa wakisimamia na kuonesha matoke mazuri fedha hizo zitatolewa.
Mradi wa miombo mara nyingi unapowekeza sehemu unataka yule anayewezeshwa au kunufaika aoneshe anamchango wa aina fulani ambapo kikundi cha Mlele kimeweza kuchangia kiasi cha shilingi milioni 7 hivyo mchango wa huu mradi unagharama ya kiasi cha shilingi mioni 240 ikiwemo mchango wa jengo la mradi.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved