Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko alipozindua madarasa 51 katika Shule ya Sekondari Lyamba yaliyojengwa kwa Fedha almaarufu Pochi la mama katika Manispaa ya Mpanda 29 Desemba 2022
Na:OMM Katavi
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Hoza Mrindoko amepokea vyumba 51 vya madarasa yaliyokamilika katika Manispaa ya Mpanda ikiwa ni maandalizi ya kupokea Wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa ajili ya muhula mpya wa masomo 2023.
Akizungumza wakati wa Hafla ya kukabidhi vyumba hivyo 51 vya madarasa almaarufu Madarasa ya Mama Samia , katika Shule ya Sekondari Lyamba Manispaa ya Mpanda Mkuu wa Mkoa Mhe.Mrindoko ameipongeza Manispaa ya Mpanda kwa kuhakikisha kukamilisha Ujenzi huo kwa wakati.
Aidha Mhe.Mrindoko pamoja na Pongezi alizotoa kwa Mhe.Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.DKT.Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa Viongozi wa ngazi zote ndani ya Manispaa ya Mpanda na Mkoa wa Katavi kwa ujumla kusimamia kikamilifu kuhakikisha kuwa watoto wote 14,904 waliochaguliwa kuripoti Shuleni kwa ajili ya kuanza masomo ya kidato cha kwanza wanaanza Masomo mapema ifikapo 9 Januari 2023 kwa kuwa hakuna kiingizio cha watoto hao kubaki Mtaani kutokana na Serikali kumaliza kabisa changamoto za uhaba wa vyumba vya Madarasa pamoja na Madawati Mkoani Katavi.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa Mrindoko amewataka Viongozi wa Kijamii mkoani Katavi kuhakikisha kuwa wanatoa hamasa ya kufanya maandalizi ya watoto waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa wakati badalam ya kusubiria mpaka shule zikifunguliwa ambapo amesisitiza kuwa hatosita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu yoyote atakayechelewesha mtoto kuripoti kidato cha kwanza.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Sophia Kumbuli akiwasilisha Taarifa yake katika Hafla ya kukabidhi vyumba hivyo vya madarasa katika Shule ya Sekondari Lyamba ameeleza kuwa Ujenzi wa vyumba 51 vya madarasa ndani ya Manispaa ya Mpanda ulianza utekelezaji wake mnamo Mwezi Oktoba 2022 ambapo Manispaa ya Mpanda ilipokea Fedha kiasi cha shilingi Bilioni 1 nje ya ukomo wa bajeti kwa ajili ya maandalizi ya mapokezi ya Wanafunzi wa Kidato cha kwanza.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved