Mkoa wa Katavi unaendelea na mkakati wake wa kuwawezesha Wajasiliamali kutambua fursa zaidi za uwekezaji na masoko katika maonesho ya Nane nane Jijiji Mbeya. Mkuu wa Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji toka Sektretariet ya Mkoa wa Katavi Mhandisi Awariywa Nnko, amewaeleza washiriki wa Maonesho ya Nane nane katika Banda la Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kuwa azma ya Mkoa wa Katavi ni kuyafanya maonesho ya nane nane mwaka 2018 kuwa ya Kilimo biashara ili yawe chachu ya mabadiliko kwa washiriki wa Mkoa wa Katavi na kuona Kilimo ni shughuli inayoweza kuboresha maisha yao. Aidha Mhandisi huyo wa Kilimo amewaambia washiriki kuwa sasa muda umefika kwa washiriki kuwa wabunifu na kujifunza teknolojia mbalimbali zinazooneshwa katika viwanja vya nane nane Jijini Mbeya na kuchukua hatua ya kuanzisha viwanda katika maeneo yao wanayotoka. “ Itapendeza na itakuwa faraja kwa wanakatavi kuona wajasiliamali walioshiriki katika maonesho haya mwaka huu 2018, mwakani wakija katika maonesho kama haya wanakuja kuonesha bidhaa zilizozalishwa na viwanda vipya walivyoanzisha wenyewe kama walivyofanya wenzetu wa Katavi Dairy Milk na RK kutoka katika Manispaa ya Mpanda, ambao tumeshuhudia wakionesha bidhaa zao zilizoongezwa thamani”.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Manispaa ya Mpanda Bibi Marietha Mlozi, amesema Halmashauri yake imejipanga kuhakikisha kuwa washiriki kutoka Manispaa ya Mpanda wanapata fursa ya kuonesha bidhaa zao na kutafuta masoko ya kudumu ya bidhaa wanazozalisha, na kubwa zaidi kujifunza kwa kina teknolojia za kilimo zinazooneshwa na taasisi na mashirika ambazo zitawasaidia kuongeza uzalishaji katika kilimo, mifugo na uvuvi. Mkuu huyo wa Idara amewaambia washiriki kuwa Halmashauri yake imejipanga kwa mwaka huu kuhakikisha inafanya vizuri katika maonesho haya, na kusema kuwa wameandaa rejista muhimu ya wajasiliamali na wakulima waliokuja kujifunza kutoka katika Halmashauri yake, rejista hiyo itatumika kuhakikisha kuwa wanamfatilia mshiriki mmoja mmoja kuona maendeleo yake baada ya kujifunza katika maonesho haya.
Naye Afisa Habari wa Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Bw.Donald amewaambia washiriki wenzake kuwa kila mtu kwa nafasi yake ajitume na ahakikishe anafanya kazi kwa bidii, ili kuhakikisha wanapata ushindi katika maonesho ya mwaka huu 2018, kwani Manispaa ndiyo Kioo cha Mkoa wa Katavi, hivyo Mnispaa ikifanya vizuri, Mkoa wote pia unakuwa umefanya vizuri.
Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda katika maonesho ya Nanenane mwaka 2018, imejipanga kuhakikisha inafanya vizuri na kuongoza katika maeneo yote.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved