Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambaye pia ni mgeni rasmi wa siku ya tatu ya Maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mhe. Charles Makongoro Nyerere, ametembelea na kukagua bidhaa mbalimbali za wajasiriamali katika banda la Manispaa ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, lililopo katika viwanja vya John Mwakangale, Jijini Mbeya.
Pamoja na kuona bidhaa za wajasiriamali wanaosindika mazao ya chakula, wafumaji, wakulima, wafugaji na wavuvi, pia alipata maelezo kuhusu namna ambavyo serikali imewezesha wajasiriamali hao kujikwamua kiuchumi.
Halmashauri zote tano za Mkoa wa Katavi, pamoja na Manispaa ya Mpanda, zinashiriki Maonesho ya Nanenane Jijini Mbeya.
Kaulimbiu: Chagua viongozi bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo, mifugo na uvuvi 2025.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved