Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amekihamasisha kikundi cha Kashaulili AMCOS kuanzisha viwanda vya kuchakata mazao ya mifugo ili kuinua uchumi wa mkoa huo.
Mhe. Mrindoko amesema hayo baada ya kukikabidhi kikundi hicho vifaa 13 vya kukamulia maziwa ya ng’ombe, mashine1 ya kuchakata chakula cha mifugo na cheti cha kusajiliwa kwake ofisini kwake Mjini Mpanda, 12/4/2023
Amesema mkoa huo unahitaji viwanda vya aina mbali mbali ikwemo viwanda vya maziwa, ngozi na nyama kwa kuwa malighafi ya viwanda hivyo ipo.
Mhe. Mrindoko ameupambanua mkoa wake kuwa ni miongoni mwa mikoa iliyo na mifugo mingi. Kulingana na sensa ya mifugo ya 2022 mkoa huo una mifugo zaidi ya Laki 8.
Amekihakikishia kikundi hicho na wananchi wote wa mkoa huo kuwa serikali yake itatoa ushirikiano mkubwa ikiwa ni pamoja na watalaam wa kusaidia kuelekeza taratibu na fedha kwa ajili ya uanzishaji wa viwanda hivyo.
Amewahimiza wananchi kujiunga na ushirika ili kuwa na sauti ya pamoja katika soko la bidhaa za mifugo na nguvu ya pamoja ya kiuchumi.
Mhe. Mrindoko amewatahadharisha Kashaulili AMCOS kutotumia vifaa walivyopewa na serikali kwa shughuli nyingine mbali na malengo ya matumizi ya vifaa hivyo.
Kashaulili AMCOS inatarajiwa kuwa mfano wa kuigwa na hamasa kwa wananchi na vikundi vingine kuchangamkia fursa mbali mbali za kiuchumi katika Mkoa wa Katavi na taifa.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe. Onesmo Buswelu amesema utoaji wa vifaa vya mifugo katika Mkoa wa Katavi ni juhudi za serikali za kuinua sekta ya mifugo nchini.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved