RC KATAVI AWAONYA MAFUNDI WA KULALAMIKA DHIDI YA SERIKALI
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe. Mwanamvua Mrindoko amewapiga stop baadhi ya wananchi wanaopenda kuilalamikia serikali badala yake watumie rasilimali zilizopo na amani iliyopo kujiletea maendeleo.
Mhe.Mrindoko amesema hayo leo katika kumbukizi la miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililofanyika kwenye viwanja vya Usevya, katika Halmashauri ya Mpimbwe, Wilaya ya Mlele.
Amesema Tanzania imejaliwa kuwa na amani na rasilimali nyingi na kuwataka watanzania kutumia rasiliamali zilizopo na fursa ya amani iliyopo ili kubadilisha hali ya maisha yao
Amezitaja kwa uchache rasilimali zilizopo nchini Tanzania kuwa ni pamoja na ardhi kubwa yenye rutuba, mito, maziwa, bahari, misitu na mbuga za wanyama.
Mhe. Mrindoko amesema Tanzania inahitaji viwanda vingi lakini viwanda mbali mbali haviwezi kupatikana kwa kuilalamikia serikali bali vitapatikana kwa kila mtanzania kufanya kazi kwa bidii na maarifa.
Amesema Muungano wa Tanzania umeleta faida nyingi sana kwa watanzania. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na usalama na utulivu, uhuru wa kuishi mahali popote Tanzania, soko la pamoja baina ya Tanganyika na Zanzibari, umeaimarisha na kuleta maendeleo makubwa katika sekta za afya, elimu, barabara na maeneo mbali mbali ya kiuchumi na kijamii.
Amewatahadhalisha watanzania kutokubali kuruhusu mtu yeyote kuvuruga muungano wa Tanzania, bali watanzania wasimame imara katika umoja na mshikamano, kuutetea na kuulinda Muungano kwa nguvu zote.
Muungano wa Tanzania ni Muungano pekee katika nchi za Afrika uliodumu karibu miongo 6 tangu kuasisiwa kwake 26/4/1964
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved