Mkuu wa Mkoa mpya wa Katavi Amos Makalaamewapa siku 14 wakuu wote wa Wilayaza Mkoa huo waandike taarifa zote za migogoro ya ardhi iliyopo kwenye Wilaya zao na hatua ambazowameisha zichukua za kutatua migogorohiyo ya ardhi .
Agizo hilo amelitoa leo wakati alipokuwa akiwatubia viongozi mbalimbali na watumishiwa Mkoa wa Katavi na wa Wilaya za Mkoa huo katika ukumbiwa Manispaa ya Mpanda mara baada yakukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuuwa Mkoahuo Meja Generali mstaafu Raphael Muhuga ambayeamestaafu .
Makala amewaagiza wakuu wa Wilaya zote tatu za Mkoa huo pamoja na wakurugenziwa Halmashauri wahakikishe ndaniya siku 14 kuanzia tarehe14/8/2018 waandike taarifa zote za migogoroya ardhi iliyopo kwenye maeneoyao na hatua ambazo wameisha chukua katika kutatua migogoro hiyona taarifa hiyo iwe imefikishwa ofisini kwakendani ya siku 14 kuanzia.
Amesema taarifa hiyo itakapo kuwa inaandaliwa wahakikishewanawashirikisha wajumbe wote wa kamatiza ulinzi na usalama walioko kwenye Wilaya zao.
Ameeleza kuwa yeye ni muuminiwa kazi za wananchi hivyo anapenda kuona kero zote za wananchi zinatatuliwa kwenye Mkoa huu ambao ameanza kuuongoza kuanzia leo baadaya kuhamishiwa hapo akitokea Mkoa wa Mbeya.
Amefafanua kuwa dirayake kubwa katika uongozi wakeni kutatua migogoro ya ardhi /kusimamia Amani na usalama kwani hayuko tayarikuacha Mkoa usiwe salama /kubororesha huduma za jamii nautii wa sheria na kuwaletea wananchi maendeleo
Amewasisitiza wakuu wa Wilaya kutenga siku mbili kila mwezikwa ajiri ya kusikiliza keroza wananchi kwani hata yeye Mkuuwa Mkoa atakuwa na sikumoja kila mwezi kwa ajiriya kusikiliza kero za wananchi .
Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wananchi ambaowalikuwa ni raia wa Nchiya Burundi na wamepewa uraia wa Tanzania wanaoishi kwenye makaziya Wakimbiziya Katumba na Mishamo waache tabiaya kujihusisha na maswala ya uhalifukwani usalama wa Nchi yetu sio wakuchezea chezea.
Mkuu wa Mkoa mstaafu Meja Jenerali Raphael Muhuga alielezakuwa amemkabidhi Mkuu huyo mpyawa Mkoa Mkoa huo ukiwa ni salama.
Amesema katika kipindi chake cha uongozi katika Mkoahuo aliyeuongoza kwa kipindicha miaka miwilina miezi minne Mkoahuo umewezakupata mafanikoa mbalimbali baadhiya mafanikio hayo ameyataja kuwa ni
Kurudisha mazingira ya Mto Katuma yaliokuwa yameharibiwana watu waliokuwa wakifanya shughuliza kibinadamu na kufugia mifugohari ambayoilikuwa ikisababisha viboko kufa kwenye hifadhiya Taifa ya Katavi kutokana na kukosa maji harihiyo kwa sasa haipo tena kwani majiya mto huo hayakauki tenawala viboko hawafi.
Mafanikio mengine ni kuongezekakwa kina cha majikatika Ziwa Rukwa ambalo kina chakekilikuwa kimepungua kutoka urefu wamita 12 hadi kufikia urefu wa kinacha urefu wa mita saba, kina hicho kimeanza kuongezeka kutokana na Mto Katuma kuingiza majikwenye ziwa hilo kwa kipindicha mwaka mzima .
Pia wameweza kuimarisha ulinzina usalama kwenye maeneo yote ya Mkoawa Katavi ambapo hapo awali kablaya yeye hajakuwa Mkuuwa Mkoa huo mabasi yoteyalikuwa hayawezi kusafiri bila kuwana eskoti ya polisiwenye silaha za moto hali hiyokwa sasa haipo mabasiyote yanayotoka na kuingiakatika mkoa wa Kataviyanasafiri bila eskoti ya polisi.
Mkoa pia umeweza kuanzishamazao mbadala ya Tumbaku baada yakuona makampuni ya ununuziwa tumbaku yamekuwayakishusha mwaka hadimwaka kilo za kununua tumbaku hivyowameanzisha mazao ya Pamba na Korosho na mwitikiowa wananchi kwenye mazao hayoumekuwa ni mkubwa
Mkoa umeweza kuanza ujenziwa Hospitaliya Mkoa ambapo mpaka sasa Mkoa mzima unayohospitali moja tuu ya Manispaaya Mpanda na ujenzi huowa hospitaliya Mkoa unafanywa chiniya ukandasasiwa SUMA JKT na tayari wameanza ujenziwa jengo la gorofa moja wodiya akina mama wajawazito.
Muhuga alisema Mkoa huowa Kataviunazo changamoto mbalimbali ambazo alizitajabaadhi kuwa ni mimba za utotoni ambapo Mkoa huo unawastaniwa asilimia 45za mimba zautotoni na kuufanya Mkoahuo kuongoza Kitaifa kwa tatizola kuwa na idadi kubwaya mimba za utotoni .
Changamoto nyingine aliitajakuwa ni Mkoa huo kuwa na idadi kubwa yawanawake wasio jua kusoma na kuandika ambapo Mkoaunawasitani wa asilimia 33 ya wanawake wasiojua kusomana kuandika hata hivyo wameisha anzakuchukua hatua za kuanzisha madarasa ya yakusoma watu wazima wasio jua kusomana kuandika .
Aliwaomba watumishi na wananchiwa Mkoa huo kumpa ushirikiano Mkuuwa Mkoa mpya kama ambavyowalivyompa yeyeili kufanya Mkoa huo uweze kupigahatua za maendeleo Zaidi .
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved