Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda imeshika nafasi ya pili katika maonesho ya Nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini na kuzawadia Kikombe na Cheti. Mshindi wa kwanza ni Manispaa ya Iringa. Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Francis Nzyungu amesema halmashauri yake imepata ushindi huo kutokana na ushirikiano mkubwa uliooneshwa miongoni mwa watumishi, madiwani na Sekretariet ya Mkoa wa Katavi. Bw.Nzyungu amesema atahakikisha kuwa wanatekeleza jukumu lao la kuwapelekea wakulima wa vijijini teknolojia na pembejeo bora ili kuongeza tija katika shughuli za uzalishaji mali na kujenga uchumi wa Viwanda katika Halmashauri yake.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved