Pichani:Makamu wa Rais Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango akikabidhi Hundi ya Shilingi Bilioni 2.3 kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko ambaye aliipokea kwa Mhe.Makamu wa Rais kwa niaba ya Wananchi katika tukio la kukabidhi hundi hiyo katika Kijiji cha Katuma Wilayani Tanganyika.
Tanganyika-Katuma
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa agizo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira kuhakikisha kuwa Elimu ya kutosha inatolewa kwa Wananchi ili waweze kutambua fursa zilizopo katika Biashara ya Hewa ukaa.
Mhe.Makamu wa Rais ametoa rai hiyo alipokabidhi hundi yenye Thamani ya Shilingi Bilioni 2.3 kwa vijiji nane katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika vinavyonufaika na Mradi wa Biashara ya Hewa Ukaa.
Akizungumza na Wakazi wa Kata ya Katuma mara baada ya kukabidhi hundi hiyo Makamu wa Rais Dkt.Mpamgo amewataka Wananchi wa Tanganyika na Mkoa wa Katavi kwa ujumla kuendelea kuhifadhi mazingira ili waendelee kunufaika na Mradi wa Hewa Ukaa ambao umewaletea maendeleo makubwa katika Sekta mbalimbali
Mhe.Dkt.Mpango ameeleza kuwa iwapo Wananchi watatuna mazingira ikiwa ni pamoja na kutunza uoto wa asili itasaidia kwa kiwango kikubwa kupungoiza ama kuondoa athari zitokanazo na mabadiliko ya Tabia ya Nchi yanayosababishwa kwa sehemum kubwa na tabia ya Wananchi kukata miti hovyo na kuharibu mazingira
Amesema ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha kuwa anatunza Mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya Nchi ambayo yamesababishwa na uharibifu mkubwa wa mazingira.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilauya ya Tanganyika Bw.Shabani Juma ameeleza kuwa Mradi wa biashara ya Hewa ukaa katika Halmashauri ya Wilayaya Tanganyika ulianza Utekelezaji wake Mwaka 2018 ukiendeshwa na Halmashauri ya Tanganyika na Kampuni ya Carbon Tanzania kwa kushirikiana na taasisi ya Tuungane
Mkurugenzi Shabani Juma ameeleza kuwa Mradi huo unatelekezwa katika Vijiji nane vya Mpembe, Kapanga,Lugonesi,Katuma,Mwese,Bujombe,pamoja na Kijiji cha Kadunda ambavyo vina Misitu yenye ukubwa wa hekta 216,944
Ameeleza kuwa tangu biashara ya hewa ukaa ianze Jumla ya Shilingi za Kitanzania Bilioni tatu Milioni Mia Tisa na Thelathini Elfu.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mpanda Vijijini Mhe.Selemani Kakoso alisema mradi wa biashara ya hewa ukaa imewanufaisha Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo amemuomba MhE.Makamu wa Rais kuingilia kati ili Misitu inayosimamiwa na Wananchi kupitia Vijiji waendelee kunufaika na Faida zitokanazo na utunzaji wa Misitu hiyo.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved