Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bibi Liliani C. Matinga ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda kwa uamuzi mzuri wa kununua gari la kuzolea taka, amesema uamuzi huo utasaidia kuhakikisha kuwa mji unakuwa safi na mahali salama pa kuishi kwani taka zikizolewa kwa wakati na kutupwa sehemu maalumu zilizopangwa itasaidia kuzuia magonjwa mbalimbali.
Pia ameitaka Manispaa hiyo kuhakikisha gari hilo linatumika kwa makusudio yake na lisitumike kwa matumizi tofauti na yalivyokusudiwa na kuishauri Halmashauri hiyo isiishie kununua gari hilo tuu kwani mahitaji ya gari la kusombea taka bado yanahitajika kutokana na jinsi Manispaa hiyo inavyokuwa kwa kasi kubwa.
Gari hilo lenye namba za usajili SM 12244 lina uwezo wa kubeba tani 16 lilikabidhiwa kwa uongozi wa Manispaa ya Mpanda ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Bibi. Lilian Matinga .
Akisoma taarifa mbele ya mgeni rasmi kwenye makabidhiano hayo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaaya Mpanda Deodatus alisema wakazi wa manispaa ya Mpanda huzalisha kiasi cha tani 70.5 za taka ngumu kwa siku sawa na tani 25,732.5 kwa mwaka ambapo asilimia kubwa ya taka hizo ni taka toka majumbani na maeneo ya biashara.
Kaimu Mkurugenzi Kangu alifafanua kuwa kutokana na upatikanaji wa lori lenye uwezo wa kubeba tani 16 litasaidia kwa kiwango kikubwa kuondoa tatizo la mrundikano wa taka ngumu zilizokuwa zinabaki kwenye viziba au kwenye maeneo yaliyoandaliwa kwa muda mrefu .
Alizitaja baadhiya changamoto zilizopo katika katika utekelezaji wa udhibiti wa taka ngumu katika Manispaa ya Mpanda kuwa ni upungufu na uchakavu wa malori ya kuzoa taka na kufafirisha taka ngumu .
Changamoto nyingine ni ongezeko la idadi ya wakazi inayopelekea ongezeko la uzalishaji wa taka ngumu na ukosefu wa dampo la kisasa kwa ajili ya uchambuzi na uzikaji wa taka ngumu.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved