Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Bi Jamila Yusuph Kimaro alipomuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko katika Ufunguzi wa Kikao cha Tathmini ya utekelezaji wa Mpango wa TASAF kilichoketi katika ukumbi wa Manispaa ya Mpanda 30 Juni 2022.
Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Mhe.Jamila Yusuph Kimaro amewaelekeza Wakurugenzi wa Halmashuri paomja na Maafisa Ugani wa Halmashauri kuwajengea uwezo Walengwa katika Mpango wa kunusuru kaya Maskini wa TASAF waweze kutumia mbinu bora na za kisasa za ufugaji ili waweze kutumia Elimu hiyo kuendeleza miradi mbalimbali wanayoianzisha.
Mhe Kimaro kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe.Mwanamvua Mrindoko, ametoa maelekezo hayo alipofungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Mkoani katavi kilichoketi katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa ya Mpanda kujadili namna ambavyo mpango huo umetekelezwa kwa kipindi cha Mwaka Mzima.
Ameeleza kuwa iwapo walengwa katika mpango wa kunusuru Kaya masikini wa TASAF watejengewa uwezo na kupewa elimu ya mbinu bora na za kisasa za ufugaji itawasaidia kwa sehemu kubwa kutumia ruzuku wanazozipata kupitia mpango huo kujikwamua na umasikini na hatimae kufikia azma ya Serikali ya kuwaondolewa Umasikini.
Aidha Mhe.Mkuu wa Wilaya huyo amewasisitiza Waratibu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Nchini TASAF Mkoani Katavi kujipanga kuhakikisha kuwa taarifa za walengwa zinapatikana na kuwasilishwa kwa wakati ili kuondoa malalamiko katika ngazi ya Jamii.
Amewapongeza Waratibu na wasimamizi wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Nchini Mkoani Katavi kwa kuhakikisha kuwa Mpango huo unaendelea kutekelezwa na kuleta matokeo yaliyokusudiwa.
Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Katavi Bi.Anna Shumbi amesema kuwa kupitia tathmini iliyofanyika imebaini kuwa Mpango wa TASAF umefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa walengwa.
Ameeleza kuwa kupitia Mpango wa TASAF Walengwa katika mpango huo wamefanikiwa kuwapeleka watoto wao Mashuleni ambapo kupitia ruzuku wanazopata zimewasaidia kuhakikisha kuwa Watoto walioko mashuleni chini ya Mpango huo wanapatiwa mahitaji muhimu kama vile Sare,Madaftari pamoja na mahitaji mengine ya Shule.
Mpango wa TASAF pia umefanikisha upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa walengwa ambapo walengwa katika moango huo wamefanikiwa kujiunga na CHF iliyoboreshwa jambo linalowahakikishia uhakika wa matibabu pindi wanapougua ameeleza Bi.Shumbi
Ameeza pia kuwa Walengwa kupitia mpango wa Kunusuru Kya Maskini TASAF Mkoani Katavi wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa katik ujenzi wa nyumbaa za gharama nafuu ukilinganisha na nyumba ambazo walikuwa wakiishi kabla hawajaingia katika Mpango.
Mpanda-Katavi (Mkoani Area)
Sanduku la Barua: Box 235, Mpanda -Katavi
simu: 025-2957108
Mobile:
Barua pepe: ras.katavi@tamisemi.go.tz
Copyright@2017 Katavi Rs. All right reserved